Chuchu: Mimi na Frank imebaki stori

STAA wa filamu za Ki­bongo, Chuchu Hans am­baye ni mzazi mwenziye na muigizaji wa kiume Vincent Kigosi ‘Ray’ amedai kuwa yeye na mzazi mwenzake Frank Mtao imebaki stori tu hivyo watu wasimhusishe naye.

 

Akizungumza na Ijumaa Wik­ienda, Chuchu alisema anachojua Frank ni mzazi mwenziye na walishamalizana muda mrefu kili­chobaki kati yake na yeye ni mtoto na si kitu kingine.

 

“Unajua nashangaa hata hayo madai ya Frank na mimi yameibu­kia wapi kwa sababu yule mtu ana familia yake na mimi nina maisha yangu mengine kabisa, sijui kwa nini watu wanapenda kuingilia familia za watu, yule na mimi imebaki stori na ni kwa sababu ya mtoto,” alisema Chuchu.

STORI: Imelda Mtema, Ijumaa Wikienda

Toa comment