CHUCHU: NILISHTUKA KUAMBIWA RAY ANANGOMA

MSANII wa ‘long time’ kwenye ‘game’ la filamu Bongo, Chuchu Hancy amefunguka kuwa hatasahau maneno aliyokuwa akiambiwa pindi alipokuwa na ujauzito wa mtoto wake Jaden kwamba ana ngoma kwa kuwa eti amepewa mimba na mwanaume ambaye ameathirika.  

 

Chuchu ambaye amezaa na muigizaji mwenzake, Vincent Kigosi ‘Ray’ alifunguka hayo hivi karibuni alipokuwa akifanyiwa mahojiano ‘exclusive’ na gazeti hili ambapo alisema, kipindi hicho alikumbana na maneno ya kuumiza ila akajipa ujasiri na hatimaye yamepita.

 

“Nilishtushwa sana na maneno hayo ila unajua siku zote mwisho wa ubaya ni aibu kwa sababu toka waseme nina Ukimwi kupitia kwa Ray mpaka leo hii bado wananiona nadunda na wala sina hata dalili yoyote ya kuumwa,” alisema Chuchu.

 

Msanii huyo aliongeza kuwa maneno hayo yaliwachukiza sana ndipo mzazi mwenziye (Ray) alipowaumbua kwa kuweka picha yake (Chuchu) mtandaoni akimnyonyesha mwanaye Jaden kuthibitisha kuwa, wote ni wazima na hapo ndipo wambeya likawashuka.

“Kuna watu wengine mpaka sasa wanaona hata aibu kunitazama, wamesahau kuwa haifai kabisa kumnyooshea mwenzako kidole,” alisema Chuchu. Ray na Chuchu wamekuwa kwenye uhusiano wa muda mrefu, ikadaiwa wana mpango wa kuoana lakini ikaonekana suala la utofauti wa dini zao limekuwa kikwazo.

 

Hata hivyo, juzikati Chuchu alisema kuwa, kwa muda mrefu ambao wamekaa pamoja, tayari ni mume na mke hivyo kilichobaki ni kuandaa sherehe kisha maisha yaendelee. “Unajua mimi na Ray tumekaa pamoja muda mrefu sana, yaani kisheria sisi tuko ndani ya ndoa, nadhani kilichobaki ni sherehe tu,” alisema Chuchu.

 

Jitihada za kumpata Ray kuzungumzia hatma yake na Chuchu na jinsi alivyokuwa akijisikia kutokana na maneno ya watu kuwa ‘anao’, hazikuzaa matunda kufuatia simu yake kutopokelewa na hata mwandishi wetu alipofunga safari hadi nyumbani kwao (ni karibu na ofisi za gazeti hili) hakupatikana. Jitihada za kumpata zinaendelea.

Stori:Imelda Mtema, RISASI MCHANGANYIKO

Loading...

Toa comment