The House of Favourite Newspapers

CHUO CHA KILIMANJARO CHASHUSHA WALIMU KUTOKA ULAYA – VIDEO

Muonekano wa KITM.

Chuo cha Kilimanjaro Institute of Technology and Management (KITM) kilichopo katika jengo la Mama Ngoma, Mwenge na Afrikasana, Sinza jijini Dar es Salaam, kimeendelea kuboresha mfumo wake wa ufundishaji kwa wananfunzi wake wa kozi mbalimbali ambapo awamu hii, kimeleta mwalimu mtaalam wa masuala ya umeme, Harry Hol kutoka nchini Uholanzi ambaye atakuwa chuoni hapo kwa muda wa wiki moja akiwafua wananfunzi wa chuo hicho wanaochukua Kozi ya Ufundi Umeme (Electrical Installations).

Harry Hol akiwa na wanafunzi wa Kozi ya Umeme chuoni hapo.

Uongozi wa chuo hicho umeamua kumleta mwalimu huyo na walimu wengine ambao watakuja baadaye, lengo likiwa ni kuwapa ujuzi wanafunzi wao waweze kuendana na soko la ajira na kuandaa wataalam wabobezi hasa katika sekta ya uchumi wa viwanda. Kozi hiyo ya umeme inatolewa chuoni hapo kwa muda mrefu na muda mfupi kuanzia miezi mitatu, sita na mwaka mmoja.

 

KITM ambacho kimesajiliwa na VETA na NACTE na kupewa namba ya usajili, REG/ANE/029, kinatoa mafunzo yake kwa vitendo ambapo walimu waliobobea, wanawafundisha wanafunzi kwa vitendo na kuwapa uwezo wa kuelewa kwa urahisi kile wanachofundishwa darasani.

Wanafunzi wa kozi ya kompyuta wakiwa darasani wakisoma kwa vitendo.

 

Kozi zingine ni Usimamizi wa Biashara (Business Management), Uhazili (Front Office and Secretarial) na Usimamizi wa Hoteli na Kuongoza Watalii (Hotel Management and Tour Guide), Accountacy na Procurement and Supply, Umeme, Kozi za Kompyuta, Graphics Designing, Video Production, Website Designing, Programming, Database, PC Maintanance, CISCO Certification, Microsoft Certification na nyingine nyingi.

Harry akimfundisha mwananfunzi kwa vitendo.

Kwa wanafunzi wa masomo ya teknolojia, chuo hicho kina maabara na vifaa vya kutosha ambapo kila mwanafunzi hupata nafasi ya kufanya kwa vitendo masomo yanayotolewa, ikiwa ni pamoja na kuunganisha mifumo ya intaneti na kamera za usalama (CCTV), huku pia kukiwa na maktaba iliyosheheni vitabu mbalimbali ambavyo ni nyenzo kubwa ya kuwaongezea maarifa na ujuzi katika taaluma zao.

 

Tofauti na vyuo vingine ambavyo ni lazima mwanafunzi alipe ada yote ndipo aendelee na masomo, KITM hutoa fursa ya wanafunzi na wazazi kulipa ada kidogokidogo kwa awamu, hivyo kuondoa usumbufu wa mwanafunzi kukosa masomo kwa sababu ya kutokamilisha ada yake.

Pia kimeendelea kutoa nafasi kwa wahitimu wahitimu wa kidato cha nne, sita na wengine ambao wangependa kujiendeleza kitaaluma katika ngazi ya cheti (certificate) na stashahada (diploma) katika kozi mbalimbali zikiwemo za mapishi,  uongozi, biashara, ufundi umeme, magari, kompyuta na udereva.

 

Nafasi hii ni kwa wahitimu wote wanaotaka kuendelea na masomo, hata kama ufaulu wao haukuwa wa kuridhisha, kufika chuoni hapo na kujadiliana na walimu wazoefu kuona jinsi ya kuwasaidia wanafunzi hao wenye nia ya dhati na masomo ili kutimiza ndoto zao.

 

Kama unahitaji mahali pa kuongezea ujuzi wako, basi Kilimanjaro Institute of Technology ndiyo chaguo lako.

Kwa mawasiliano;

Simu: +255 717 816034 / +255 766 348652
Email: [email protected]

KWA MAELEZO ZAIDI TEMBELEA ==> Kilimanjaro Institute of Technology and Management (KITM)

KIBOKO YAO! Chuo Cha Kilimanjaro Chaleta Mkufunzi MZUNGU!

Comments are closed.