CHUO CHA KITM CHAHAMIA GHOROFA JIPYA, CHATANGAZA NEEMA
Chuo cha Kilimanjaro Institute of Technology and Management (KITM) ambacho awali makao makuu yake yalikuwa katika Jengo la Hospitali ya Mama Ngoma, Mwenge jijini Dar es Salaam, kimehamia kwenye jengo jipya la kisasa lenye ghorofa tano, lililopo mkabala na maghorofa ya Jeshi la Wananchi (JWTZ), Mwenge, jirani na kilipokuwa awali.
Mbali na kuuanza mwaka katika jengo hilo jipya la kisasa, pia kimeendelea kutangaza ofa ya nguvu kwa wahitimu wa kidato cha nne na watu wengine ambao wangependa kujiendeleza kitaaluma katika ngazi ya cheti (certificate) na astashahada (diploma) katika nyanja mbalimbali.
Chuo hicho kinachofundisha masomo ya teknolojia ya mawasiliano, biashara, uhasibu na ufundi, kimeendelea kujipatia sifa za kipekee kutokana na wahitimu kutoka chuoni hapo, kuendelea kufanya vyema katika soko la ajira.
Kozi zinazofundishwa na walimu wazoefu chuoni hapo, ni pamoja na Teknolojia ya Mawasiliano (ICT), Usimamizi wa Biashara (Business Management), Uhazili (Front Office and Secretarial) na Usimamizi wa Hoteli na Kuongoza Watalii (Hotel Management and Tour Guide), Accountacy na Procurement and Supply.
Chuo hicho kilichosajiliwa na VETA na NACTE na kupewa namba ya usajili, REG/ANE/029, kinatoa mafunzo yake kwa vitendo ambapo walimu waliobobea, wanawafundisha wanafunzi kwa vitendo na kuwapa uwezo wa kuelewa kwa urahisi kile wanachofundishwa darasani.
Kwa wanafunzi wa masomo ya teknolojia, chuo hicho kina maabara na vifaa vya kutosha ambapo kila mwanafunzi hupata nafasi ya kufanyia kwa vitendo masomo yanayotolewa, ikiwa ni pamoja na kufanyia marekebisho kompyuta kwa vitendo, kuunganisha mifumo ya intaneti na kamera za usalama (CCTV), huku pia kukiwa na maktaba iliyosheheni vitabu mbalimbali.
Kwa upande wa wanafunzi wanaosomea masomo ya hoteli na kuongoza watalii, chuo hicho kina utaratibu maalum wa kuwapeleka wanafunzi wake kufanya mazoezi kwa vitendo kwenye hoteli kubwakubwa, na hivyo kuwaongezea ‘exposure’ na uelewa wa kile wanachofundishwa darasani.
Tofauti na vyuo vingine ambavyo ni lazima mwanafunzi alipe karo yote ndiyo aendelee na masomo, KITM hutoa fursa ya wanafunzi na wazazi kulipa ada kidogokidogo kwa awamu, hivyo kuondoa usumbufu wa mwanafunzi kukosa masomo kwa sababu ya kutokamilisha karo.
Vyeti vinavyotolewa kwa wahitimu wa cheti hicho, vinatambulika na vyuo vingine vikubwa nchini pamoja na vile vya nje ya nchi, hivyo kuwapa urahisi wanafunzi wanaopenda kuendelea na masomo ya juu zaidi, ndani ya nje ya nchi na pia kupata ajira kwa urahisi kwa wale wanaotaka kuingia kwenye ajira.
Kwa kuzingatia uhitaji wa waajiriwa wanaohitaji kujiendelea kimasomo, chuo hicho pia kinatoa mafunzo maalum ya jioni (evening programs) ambapo kwa wale wanaofanya kazi, wanaweza kuingia darasani baada ya muda wa kazi na kufundishwa na walimu wazoefu hivyo kuokoa muda.
Pia chuo hicho kimezindua kozi nyingine mpya ambazo ni pamoja na Electrical Installation (Ufundi Umeme) na Video Production, wakitumia kaulimbinu yao ya ‘KITM Elimu Na Ujuzi Kwa Maendeleo Ya Viwanda’. Kama unahitaji mahali pa kuongezea ujuzi wako, basi Kilimanjaro Institute of Technology ndiyo chaguo lako.
Na Mwandishi Wetu
Kwa mawasiliano;
- Email: [email protected]
Comments are closed.