The House of Favourite Newspapers

Chura Aliyevunja Rekodi Kwa Ukubwa Apatikana Australia Akiwa na Uzito wa Kilo 2.7

0

Chura mkubwa zaidi ambaye maofisa wa wanyama-pori walifikiri ni bandia amepatikana katika msitu wa mvua kaskazini mwa Australia.

Chura huyo ni mkubwa mara sita kuliko wa kawaida, ana uzito wa kilo 2.7 na anaweza kuvunja rekodi ya dunia.

Chura huyo aliyepewa jina “Toadzilla”, mara moja aliwekwa kwenye chombo na kuondolewa porini.

Chura – ambao waliletwa Australia kwa mara ya kwanza mnamo 1935 – ni moja ya wadudu waharibifu zaidi nchini humo na sasa wanakadiriwa kuwa zaidi ya bilioni 2.

Wakati mlinzi wa bustani hiyo Kylee Gray alipomwona mnyama huyo mkubwa kwa mara ya kwanza akiwa kwenye doria huko Queensland, hakuamini macho yake.

“Sijawahi kuona chura mkubwa hivyo,” aliambia Shirika la Utangazaji la Australia.

“Alionekana kama mpira wa kandanda wenye miguu. Tulimuita Toadzilla.”

Timu yake ilimkamata haraka Toadzilla – anayeaminika kuwa mwanamke – na kurejea kwenye kituo cha bustani hiyo kwenda kumpima.

Walijua angekuwa mzito, lakini walishangaa kupata kwamba angeweza kuweka rekodi mpya ya dunia.

Rekodi ya sasa ya Dunia ya Guinness kwa chura mkubwa zaidi – ni uzito wa 2.65kg – iliyowekwa na chura wa Uswidi aitwaye Prinsen mnamo 1991.

Bi Gray anasema spishi hii kubwa inaweza kuwa iliacha kula lishe ya kawaida ya wadudu, wanyama watambaao na mamalia wadogo.

“Chura wa ukubwa huo atakula chochote kinachoweza kutoshea mdomoni mwake,” alisema.

Leave A Reply