The House of Favourite Newspapers

Chuzi Ndo Hilo, Hakuna Kuonja!-11

0

ILIPOISHIA GAZETI LA IJUMAA WIKIENDA:

“Mh! Au uliwahi kutembea na mke wa mtu ukachezewa?”

“Hapana. Sijawahi.”

“Mh! Yaani hata dakika tano hufiki? Afadhali ungekuwa unafika hata dakika tano tu na mimi ningejitahidi.”

“Looh!,” alisema Musa huku akiwa amelala akiangalia juu kwenye dari.

“Loo nini sasa?” aliuliza mama Shua, akaendelea…

TAMBAA NAYO SASA…

Kama unaumwa sema usaidiwe.”

“Mimi siumwi.”

“Sasa kama huumwi kwa nini unashindwa kuwa mwanaume barabara kama wenzako?”

Swali hilo lilimuumiza sana Musa, akatoka kitandani haraka, akaenda bafuni kuoga. Mama Shua akajua akirudi wataendelea, lakini cha ajabu Musa aliporudi akashika nguo zake na kuvaa…

“Mimi nakwenda home.”

“Ha! Wewe, yaani nimeacha kazi kwa ajili yako halafu unasema unakwenda home, mimi unaniachaje sasa?”

“Unataka nikupe shilingi ngapi?”

“Sitaki hela, njoo kitandani bwana. Mbona unaonekana kijana mzuri, mtanashati, rijali lakini unashindwa na kitu kitogo sana?! Yaani haya mapaja yangu hayakupi uwezo Musa? Ona yalivyo mazuri, angalia kifua changu…”

“Noo mama Shua. Acha maneno yako ya kejeli. Unaniumiza sana,” alisema Musa akijiandaa kuvaa ili kutoka zake.

Uso ulimpwaya, muda mwingi aliangalia pembeni au chini ili kukwepa kukutana macho na mwanamke huyo. Alitamani angeumbwa mwanamke kwani angekwepa kudhalilishwa kule…

“Ukisikia mwanaume kapata aibu basi hii yangu ni namba moja, laiti ningejua yangetokea haya wala nisingemkubalia mama Shua tukutane hapa gesti,” Musa aliwaza.

“Musa,” aliita mama Shua…

“Mm…”

“Hebu kaa hapa kitandani,” mama Shua alisema kwa sauti kama yenye amri.

Musa alikaa huku bado akiangalia chini…

“Hebu niambie tatizo lako kwa uwazi kabisa, naamini naweza kukusaidia. Haiwezekani kijana mzuri kama wewe udhalilike mbele ya mwanamke.”

“Tatizo langu unalijua…”

“Mimi silijui, uliniambia lini?”

“Kwani huoni kama nashindwa kumudu kuwa uwanjani hata kwa dakika mbili?” alisema Musa huku machozi yakimlengalenga…

“Lengo langu nataka kujua huwa unajisikiaje mpaka unashindwa kuwa uwanjani kwa muda hata huo?”

“Inatokea tu. Mi mwenyewe sijui.”

“Tangu lini?”

“Tangu nianze kujua kusakata kabumbu uwanjani.”

“Lo! Kwa hiyo mademu zako wote wanakumbana na kisanga hicho?”

Musa, awali alisita kujibu kisha akasema…

“Ndiyo.”

“Mh! Kwani huwa unakuwa na kiu sana kabla ya kuingia uwanjani?”

“Sana. Ndiyo maana hata wewe ulivyoingia tu nikakuvamia,” alisema Musa. Sasa kidogo aibu ilianza kumtoka, alihisi anaweza kupata ufumbuzi kwani katika mademu wake wote waliommwaga kwa sababu ya udhaifu huo hakuna aliyeonesha dalili ya msaada…

“Mimi nitakusaidia Musa…”

“Kwa njia gani?” Musa aliuliza haraka huku kwa mara ya kwanza tangu kutomudu mchezo, aligeuka kumwangalia mwanamke huyo.

Mama Shua akiwa bado kitandani, alimvutia kwake Musa akamlaza huku akimbembeleza kwa maneno mazuri ya mahaba…

“Nakupenda sana mpenzi wangu, umetokea kuwa usingizi wangu. Nikiwa kitandani nikakuwaza wewe huwa nalala usingizi usio na jinamizi.”

Musa alichaji upya, akajikuta ana nguvu za ajabu, akaamini safari hii ushindi ni wake. Alichojoa akatupa kule, akaingia uwanjani na mama Shua…

“Lakini mimi bwana nina wasiwasi wewe una wanawake wengi,” alisema mama Shua wakati mechi ikianza upya…

“Mimi sina mwanamke…”

“Je, siku nikijua unao?”

“Amua chochote kile.”

“Mmm! Wewe Musa hujatulia wewe…mimi najua…na kama kweli una wanawake wengine naomba achana na mimi kabisa.”

“Kweli mimi sina wanawake mama Shua. Niamini mimi…wanawake wenyewe wakishajua niko hivi wakiondoka wanafuta namba yangu kwenye simu zao.”

“Nitafuatilia, maana mimi sitaki Ukimwi.”

Maneno ya mama Shua yalimkata stimu Musa kiasi kwamba akajikuta anacheza mechi bila akili yake kuwepo pale hivyo dakika zikakatika…

“Ina maana unahisi mimi naweza kuwa na virusi vya Ukimwi siyo?”

“Inawezekana, mimi nitajuaje?”

“Sasa mbona umekubali bila kutumia zana kama una wasiwasi?” aliuliza Musa akikosa mudi kabisa.

“Nimejitolea kufa kwa ajili yako.”

Wakati wanazungumza hayo, mama Shua alishika kasi, akajikuta anashikwa na kigugumizi huku akibadilisha maneno, sasa yakaja yale ya mahaba, Musa naye ikawa kama amezinduka kutoka kwenye maneno ya kero ya mwanamke huyo na kurudia hisia za mahaba, akatangaza anavunja dafu sambamba na mama Shua, wakavunja wote.

Musa alishtuka, kwamba alichukua zaidi ya dakika kumi wakati wa kujibu maswali magumu ya mama Shua huku wakiwa wanaendelea na mechi…

“Oooh! Oooph!” alihema sana Musa…

“Tumetumia dakika ngapi baby?”

“Kama kumi hivi…”

“Nooo baby! Dakika kumi na mbili kamili.”

“Haa! Kwa mara ya kwanza baby…ni kwa nini? Kwani umenitibu kwa dawa gani? Mbona sijaona kitu?” aliuliza Musa uso wake ukiwa umechangamka kwa furaha…

“Unajua wewe unakosea kitu kimoja,” alisema mwanamke huyo lakini mara simu ya mume wake ikaita, akaomba kuipokea…

“Pokea baby,” alisema Musa…

“Haloo…”

“Umetoka kazini muda mrefu, umekwenda wapi mama Shua? Niambie ukweli.”

Je, nini kitaendelea hapo? Usikose kusoma kwenye Gazeti la Ijumaa Wikienda, siku ya Jumatatu.

JIUNGE NA GLOBAL BREAKING NEWS
GLOBALBREAKINGNEWS.JPG

Leave A Reply