Chuzi Ndo Hilo, Hakuna Kuonja!-16

ILIPOISHIA GAZETI LA IJUMAA:
“Tangulia na mimi natoka hapa nakwenda chukua gari kisha hotelini, hapa nilipo mawazo yangu yote nipo na wewe kitandani.”
ENDELEA NAYO MWENYEWE…

Mama Shua alizidi kusisimka mwili, hata maneno ya mumewe akayaweka pembeni kwanza…
“Basi baby usichelewe bwana,” alisema mama Shua huku akihisi kuchelewa kufika kwenye hiyo hoteli.

Alifika, akazama ndani huku mikono ikibonyeza vitufe vya simu kumtaarifu Musa kwamba ameshafika eneo la tukio…
“Baby, nipo eneo la tukio tayari.”
Musa alitoka kama swala, akafika hotelini ndani ya dakika chake…
“Umechukua rum?”
“Kilekile.”
“Oke.”

Mlango ulisukumwa, Musa alizama ndani na kumkuta mama Shua ameshavua kila kitu na yupo na suti ya ngozi tu…

“Du! Baby unanihamasisha siyo?” alisema Musa akimwangalia mama Shua kwa macho yaliyojaa tafsiri ya ‘mahaba niondolee uhai wangu’.

Musa, kwa kasi ya mashine ya cherehani alivua suruali, akatupa huko, akachua shati akatupa kule, akavua boksa akaivurumishia mbali, akachojoa singilendi na kuirushia mbali, akapanda kitandani huku akichekacheka lakini moyoni alipokumbuka kwamba anaweza kuchemsha licha ya mbwembwe nyingi alijikuta akikosa nguvu ghafla…

“Daa! Inawezekana lakini…sijui mganga gani atanisaidia mimi?” alisema moyoni Musa.
Mama Shua kwa kujua kuwa Musa ana ‘ugonjwa’ wa kumaliza haraka, alimdaka, akampa mabusu motomoto huku akimsema kwamba amechelewa…
“Hivi kwa nini umechelewa baby lakini?”

“Mh! Mbona nimewahi darling…”
“Hakuna bwana, yaani mpaka uongee na wanawake wako wee ndiyo uje kwangu.”
“Sikuwa na mwanamke baby, ndiyo maana nilikuita pale. Sasa kama ningekuwa na mwanamke ningesema uje? Acha mawazo yako hayo.”

Muda wote wa mazungumzo, wawili hao walikuwa wakishikana sehemu mbalimbali za mwili huku wamelala. Musa alichaji sana lakini kule kupambana na lawama za mama Shua kulianza kumkatisha tamaa kwa mbali…

“Lakini baby mbona umekuwa mtu wa lawama sana? Huniamini, huniachii nafasi ya kufurahia tukio, vipi kwani?” alilalamika Musa…

“Sikuamini ndiyo, sasa wewe unanisaliti hivihivi naona halafu nikuache kweli?”
Ilifika wakati, mama Shua akiwa anaendelea kumlaumu Musa, mechi ikaanza pamoja na lawama zake juu…

“Nikwambie kitu kimoja baby, mimi sipendi kabisa usaliti. Usaliti utanifanya mimi na wewe tuachane kabisa,” alisema mama Shua huku mechi imeshaanza…
“Mimi sikusaliti mpenzi wangu, hayo mawazo yatupilie kwa mbali. Nakupenda wewe, nakupenda sana.”

Mama Shua hakuacha kumtuhumu Musa kwa usaliti mpaka Musa akajikuta anachukua dakika kumi na tatu hivi akiwa bado uwanjani, ndipo mwanamke huyo akaamua kuachana na lawama na kumsifikia kwa mahaba anayompa, Musa akajikuta anamaliza mchezo, wakamaliza sambamba.
Sasa walikuwa wamelala wakiangalia juu huku wote wakihema kwa sana…
“Hivi baby mbona kama lile tatizo halipo, we unatumia dawa gani?”
“Naijua mwenyewe, wala sikwambii ng’o.”
“Niambie kidogo baby jamani.”

“Sikwambii ng’o na hiyo dawa naijua mwenyewe. Ukienda kwa mwanamke mwingine utaipata ile hali, dakika moja tu mpira umeisha, aibu kwako,” alisema mama Shua huku akigeuka kumwangalia Musa kwa macho ya utani.
***
Simu ya baba Shua iliita, mama Shua alipoiangalia, akasonya kisha akaacha bila kuipokea…
“Huyu naye,” alisema moyoni mama Shua…
“Mbona hupokei, nani kwani?”
“Mista.”

Musa aliposikia ni mista, damu zikamkimbia mwilini, alihisi baba Shua amesimama mlangoni na kupiga simu ya mkewe…
“Mh! Atakuwa wapi?” aliuliza Musa…
“Mi sijui.”

“Siyo kwamba yupo hapo nje kweli!”
“Nje ya mlangoni?”
“Ndiyo.”

“Hawezi. Namjua yule. Ajue mimi nipo ndani humu halafu asimame na kupiga simu! Angeingia na mlango mpaka ndani.”
Mara ikaingia meseji…
“Umekwenda hospitali gani?”
Mama Shua hakuijibu meseji hiyo kwani ilikuwa ngumu kwake kueleza. Angeitaja si ina maana mumewe angemfuata!
***
Baada ya mapumziko ya kama lisaa limoja, mama Shua akataka mechi tena, akamfanyia vilevile Musa na mechi ikaanza kwa uzuri mpaka dakika ya kumi, Musa akamaliza.
Walikaa ndani ya hoteli hiyo mpaka saa kumi na nusu. Musa ndiye aliyeanza kutoka hadi kwenye gari, akafungua mlango na kuzama ndani, akamtumia meseji mama Shua…
“Njoo, kuko shwari.”

Mama Shua naye akachomoka mpaka kwenye gari ambapo alikuta mlango wa upande wa abiria upo wazi.

Musa aliwasha gari, wakaondoka.
“Sasa utashukia wapi?” aliuliza Musa…
“Mh! Jirani na kile kituo, saa hizi najua yeye atakuwa ameshafika nyumbani,” alisema mama Shua.

Musa aliegesha gari pembeni, mama Shua akashuka na kuanza kutembea polepole.
Musa naye alipanda kaukuta na kulipeleka gari anapolilaza. Baba Shua alikuwa akienda dukani, akakutana na mama Shua, lakini pia akaliona gari la Musa na Musa mwenyewe akishuka, akashtuka…

Loading...

Toa comment