Chuzi ndo hilo, hakuna kuonja!-20
ILIPOISHIA GAZETI LA IJUMAA:
“Hivi baba Shua mimi naumwa hata kuniuliza hutaki? Hayo ni mapenzi gani lakini? Ina maana wewe uumwe mimi nikae kimya nakuangalia tu utajisikiaje?”
“Kama unaumwa si ungeenda hospitali?”
“Kwani sijaenda?”
“Pale gesti Makumbusho ndiyo hospitali?”
SHUKA NAYO MWENYEWE SASA…
Mama Shua alishtuka sana kumsikia mumewe akisema hivyo, akajikuta anamtumbulia macho.
Kusema amuulize kama alimwona alishindwa kwani alijua lazima mumewe amemwona akiingia au akitoka kwenye gesti hiyo ya Makumbusho…
“Au kama hajaniona yeye kuna mtu amemwambia,” alisema moyoni mama Shua huku akiwa na uso wa aibu…
“Da! Nimeumbuka hivihivi…yaani hapa napotea huku najiona,” mama Shua aliendelea kusema moyoni na kuingia chumbani huku miguu yake ikikosa nguvu ya kutembea…
“Hizi salam zikifika kwa mama ndiyo tabu,” aliendelea kusema moyoni mama Shua huku akilitupa begi lake chini.
Jambo lililomshangaza sana ni kuona mumewe amelichukulia suala la yeye kuingia gesti Makumbusho kama utani…
“Ina maana awe ameniona au ameambiwa halafu aniulize kirahisi vile? Haiwezekani,” alisema moyoni.
Baba Shua aliendelea kukaa sebuleni bila kumfuata mumewe chumbani, alikuwa akiwaza…
“Huyu dawa yake ni moja tu. Ni kumtema. Nikisema nimvumilie nitakufa kwa presha. Hivi kwa nini ananifanya mimi mtoto mdogo? Atakapokuwa mbali na mimi ndiyo atajua umuhimu wa kuheshimu ndoa yake.”
***
Kule chumbani, mama Shua alikaa kitandani akiendelea kuwaza na kujiuliza maswali kadhaa kichwani…
“Na kama aliniona yeye mwenyewe si ina maana aliniona nikiwa na Musa? Da! Nimeumbuka kwelikweli.”
***
Musa naye alikuwa chumbani kwake. Alihisi joto la mahaba, akatamani amwite mama Shua walicheze libeneke ili alale usingizi mnono. Akamtumia meseji…
“Baby.”
Mama Shua hakuchukua muda kuijibu meseji hiyo, tena kwa haraka sana…
“Niambie baby! Siko poa sana.”
“Pole baby, unaumwa?”
“Hapana… basi tu.”
“Sasa si uje, nimekumisi sana.”
“Da! Musa bwana…unanipa majaribu ujue.”
“Kwa nini?”
“Si hivyo unavyoniita…mista yupo ujue…”
“Kha! Kwani hata juzi si alikuwepo…mbona ulikuja…njoo bwana…mara moja tu…”
Mama Shua hakumjibu Musa, akavua nguo na kuvaa upande mmoja wa kanga huku moyoni akisema…
“Musa naye…yaani kila saa anataka.”
Alitoka sebuleni, akamkuta mumewe amekaza macho kwenye tivii akiangalia taarifa ya habari, akatoka kwenda uani.
Aliweka maji bafuni, akasimama kwa muda akiwaza akaingie chumbani kwa Musa au la!
“Lo! Mbona shughuli…lakini na mimi kama namuhitaji Musa…ngoja nimwambie awe tayaritayari ili nikifika tu chapuchapu ili niwahi kutoka.”
Alirudi chumbani, akamtumia meseji Musa…
“Baby, mlango uwe tayari na wewe pia uwe tayari…nikifika tu chapuchapu ili nitoke.”
“Poa,” alijibu Musa.
Mama Shua alitoka, akajifanya anakwenda uani. Akasimama kwenye mlango wa Musa, akashika kitasa, akafungua, akazama ndani…
“Baby yaani hapa hakuna kupoteza muda, jamaa amekaa sebuleni.”
“Poapoa,” alisema Musa huku akifunga mlango.
Mama Shua alijivua ile kanga na kuitupia kwenye kiti, akajipeleka kitandani mwenyewe huku akiwa anahema kwa kasi.
Hakukuwa na maandalizi wala kupandishana joto, waliingia uwanjani moja kwa moja na kuanza kulisakata kabumbu harakaharaka. Safari hii, mama Shua hakuwa na haja ya kumsemesha Musa ili achelewe matokeo yake akamhamasisha ili amalize mchezo haraka. Kweli ikawa hivyo tena wote kwa pamoja.
Baada ya hapo, mama Shua aliiokota kanga yake haraka, akajifunga kifuani na kutoka kinyemela huku akiurudishia mlango polepole ili usisikike.
Alishtuka kumsikia mumewe anaoga yale maji aliyoyaweka yeye…
“Mh! Ina maana…si atajiuliza mimi niko wapi?” alijiuliza mwenyewe mama Shua huku akitetemeka.
Alikwenda chumbani, akakuta nguo za mumewe ziko chini…
“Ina maana hapa atajua nilikuwa wapi! Chooni ndiyo bafuni kulekule. Jiko liko ndani na limefungwa. Na kama ni jikoni alipokuwa akienda kuoga si angeniona. Da!”
Alishika simu yake, akamtumia meseji Musa…
“Da! Nahisi kama nimeumbuka.”
“Kivipi baby, nikupigie simu?”
“Hapana! Ila kuna ishu kubwa sana.”
“Da! Baby, unanitisha. Jamaa kajua?”
“Atakuwa kajua.”
Mara, baba Shua aliingia akitokea bafuni kuoga. Akajifuta maji kwa taulo, akavaa bukta kisha akatoka kwenda kukaa sebuleni…
“Mh! Ina maana hajajua? Mbona haniulizi?”
Mama Shua naye akatoka kwenda kutenga maji mengine akaoga na kurudi chumbani.
Hakuwa na namna, alipanda kitandani kulala huku moyo ukimwenda kwa kasi ya ajabu…
“Lakini mimi nimeanzisha tabia gani jamani? Mbona zamani sikuwa hivi, sasa itakuaje?”
Alipitiwa na usingizi. Alipokuja kuamka, mumewe alikuwa pembeni amelala akiangalia juu na magoti yakiwa juu kwa maana kwamba hakuwa usingizini…
“Baba Shua…”
“Mm…”
“Mbona hujalala?”
“Ungekuwa wewe ungelala?”
“Ningekuwa mimi kivipi sasa?”
“Wewe ungekuwa umeniona mimi nikiingia chumbani kwa mwanamke mpangaji mwenzetu na ukasikia kitanda kinalia na mimi natoa sauti za mihemko ya mapenzi ungepata usingizi?”