The House of Favourite Newspapers

Chuzi Ndo Hilo, Hakuna Kuonja!-21

0

ILIPOISHIA GAZETI LA IJUMAA WIKIENDA:

“Natoka kazini napitia kwa rafiki yangu Rukia… kuna ishu ya kuzungumza naye…”

Hakujibiwa meseji hiyo lakini yeye hakujali, akamgeukia Musa…

“Mimi nimeshafika, wewe uko wapi baby?”

“Nakaribia baby,” alijibu Musa.

Mara, ikaingia meseji nyingine. Hii ilitoka kwa mama yake kijijini…

“Kwa hiyo hiyo hoteli ndiyo umeigeuza nyumbani kwako sasa??!!”

SHUKA NAYO SASA…

Mama Shua alijikuta akiingia wasiwasi, akatoka kwa kasi huku macho pima…

“Mungu wangu…Mungu wangu. Yule  mzee kaniona tena jamani, kamtumia mama meseji,” alisema moyoni mama Shua huku akiseti simu yake ili ampigie mdogo wake…

“Selina, mama kanitumia ujumbe tena. Inaonekana yule mzee ameniona tena. Mimi nilikuja hapa kuonana na mwanamke mwenzangu, wala si Musa…”

“Musa ni nani kwani dada?” mdogo wake alimuuliza.

“Ha! Nilikosea.”

Mama Shua alikata simu, akatoka hadi nje kabisa na kusimamisha teksi tayari kwa kurudi nyumbani kwake.

“Hivi yule mzee ananitafuta nini mimi? Ana maana gani kunifuatilia kiasi hiki?” alijiuliza akiwa anapanda kwenye gari hilo.

Alisahau kabisa kumpigia simu Musa kumjulisha mpaka Musa alipopiga yeye…

“Uko wapi baby?”

“Ah! Baby nimepata dharura bwana, nimeondoka. Please tukutane kesho baby au nyumbani nitakwambia.”

“He! Dharura gani mpaka unafikia hatua ya kuondoka bila kuniambia mapema. Mimi nimeingia mpaka hotelini sasa.”

“Sikia Musa, twende kwingine tukatafute hoteli nyingine.”

“Kama wapi?”

“Popote pale lakini si hapo,” alisema mama Shua na kukata simu ili asome meseji ambayo iliingia wakati anaongea na Musa…

“Umeona aibu kuingia hotelini na kuamua kuondoka siyo? Ungeingia tu. We mtoto huo mwenendo wako kama utaendelea kuwa hivyo sijui kama utadumu kwenye ndoa,” ni ujumbe uliotoka kwa mama yake.

Mama Shua aliishiwa nguvu kabisa kiasi kwamba alitamani ardhi ipasuke sasa ili afie humo.

Mara, Musa akampigia simu…

“Haloo Musa…”

“Ee, sasa sikia. Nakwenda Makumbusho, tukutane kule,” alisema Musa…

“Sawa. Sehemu gani?”

“Pale baa. Lakini tukitoka pale tunakwenda gesti, sawa?”

“Sawa baby.”

Mama Shua alihisi mwili unamsisimka kwa maneno ya Musa, akajikuta anaachana na wazo la kwenda nyumbani. Akamwambia dereva ampeleke Makumbusho.

Alifika Makumbusho, akashuka. Akatembea hadi kwenye baa hiyo lakini hakumkuta Musa, akampigia simu.

“Uko wapi sasa, mbona hapa baa haupo?”

“Nilikuja kuchukua chumba huku gesti.”

“Wapi nije?”

Musa alimwelekeza mama Shua. Wakati anakwenda, njiani mama Shua alikasirika sana kuhusu yule mzee na mama yake hivyo akaamua moyoni kwamba akikutana na Musa ampe mahaba mazito kama kulipa kisasi kwa mama yake na yule mzee.

Mama Shua aliingia, akapita kwenye korido mpaka kwenye chumba kwa mujibu wa maelekezo ya Musa. Akazama ndani.

Ile anafika tu, akiwa bado amesimama alimkumbatia Musa na kumpiga mabusu kibao, mara akaomba denda, wakazama kwenye denda kwa muda wa kama dakika tano nzima huku wakitoa miguno ya mmmh…mmmh!

Mama Shua, wakiwa bado wamesimama, akapeleka mkono kwenye suruali ya Musa na kuanza kumfungua kizuio chake kisha akamshusha suruali hadi chini.

Baada ya hapo akamvua shati, mara akamvua singilendi mpaka Musa akabaki mweupe.

Musa naye kuona hivyo, akaanza na yeye mpaka mama Shua akabaki mweupe kama yeye. Wote wakabaki weupe, wakapanda kitandani.

Mama Shua alikuwa akihema sana hivyo kumfanya Musa naye kuambukizwa na mhemo wake, hawakuchukua muda wakaingia kwenye uwanja na kuanza kucheza.

Mama Musa huku akijua kwamba Musa atafika haraka safari yake ilibidi aanze kumsemesha…

“Unajua mwenzako nina msala…”

“Msala gani?”

“Mama angu amejua mimi ninaingia hotelini pale. Kuna mtu ananionaga. Sasa leo pia kaniona. Akamwambia mama, mama akanitumia meseji nzito sana. Yaani jamani.”

“Mh! Kwa hiyo?”

“Kwa hiyo nini sasa. Nilitaka kwenda nyumbani lakini nikajua wewe utakwenda pale na wanawake zako.”

“Umeanza baby. Kwa nini tusisubiri tumalize ndiyo uanze kunishutumu?”

“Hakuna bwana, we unapenda sana wanawake. Mi unanikera sana ujue.”

“Uliwahi kuniona na mwanamke wapi?”

“Najua tu. We endelea.”

Ilifika dakika ya kumi siku hiyo, mama Shua ndiyo aliyeanza kutangaza nia kwa Musa ikabidi Musa naye ahemuke na kutangaza na yeye wakafika mwisho wa  mchezo.

***

Waliendelea kulala humo chumbani huku mama Shua akimtekenyatekenya Musa mpaka Musa akawa ngangari tena. Wakaingia tena uwanjani. Safari hii, mama Shua alimsemesha sana Musa maneno ya kila aina…

“Siku nikikuona na mwanamke mwingine Musa utanijua mimi ni nani!”

“Kivipi?”

“Nitakufanyia fujo hata mbele za watu mimi sitajali ujue…ohooo.”

“Haitatokea.”

“Haitatokea kwa sababu unajificha sana si ndiyo?”

“Hamna,” alisema Musa hapohapo akatangaza nia.

***

Mama Shua aliingia nyumbani akijifanya mnyonge kwamba, hajisikii vizuri maana alimkuta mume wake amesharudi na amekaa sebuleni. Lakini mumewe hakumuuliza mbona mnyonge, alimwangalia tu.

“Hivi baba Shua mimi naumwa hata kuniuliza hutaki? Hayo ni mapenzi gani lakini? Ina maana wewe uumwe mimi nikae kimya nakuangalia tu utajisikiaje?”

“Kama unaumwa si ungeenda hospitali?”

“Kwani sijaenda?”

“Pale gesti Makumbusho ndiyo hospitali?”

Je, nini kitaendelea hapo? Usikose kusoma kwenye Gazeti la Ijumaa Wikienda, siku ya Jumatatu.

Leave A Reply