The House of Favourite Newspapers

Chuzi Ndo Hilo, Hakuna Kuonja!-31

0

ILIPOISHIA IJUMAA WIKIENDA:

“Hapahapa…tena wale pale wamekaa. Hebu ingia na sisi tukakae tuone,” alishauri Jome, baba Shua akaingiza gari kwenye maegesho ya hoteli hiyo na kupaki sanjari na gari la Musa, wakashuka wote.

JIACHIE MWENYEWE…

Walikwenda kukaa nyuma ya meza waliyokaa mama Shua na Musa na walipokaa, Musa aliwaona kwa sababu aliwafesi, mama Shua aliwapa mgongo…

“Mama Shua tumekwisha…mume wako na jamaa mwingine wamekaa nyuma yako,” alisema Musa kwa sauti ya chini huku akiangalia sakafuni kwa aibu kubwa…

“Wewe Musa…unasema kweli?” aliuliza mama Shua…

“Mungu vile! Halafu inaonekana wamejua wewe upo hapa. Na mbaya zaidi walipokaa, huwezi kukimbia wala kufanya lolote zaidi ya kuonekana.

Baba Shua, kwa hasira kubwa aliamua kumpigia simu Maua na kumwelekeza alipo kisha akamuuliza kama anaweza kumfuata…

“Jamani kwa nini nisije? Nakuja sasa hivi…” alisema Maua…

“Chukua teksi nitalipa,” alisema baba Shua…

“Teksi ya nini? Nachukua bodaboda tu…”

“Ha! Jamani mke wangu, yaani uchukue bodaboda kweli wakati gari lipo ndiyo maana kwa hadhi yako nikasema uchukue teksi…”

Benny bwana, mimi kuwa na hicho kigari si kwamba nina hadhi ya juu, niko sawa tu mbona. Nakuja sasa hivi.”

Baba Shua alimsimulia Jome kwamba, Maua atafikia pale muda si mrefu…

“Safi sana…safi sana…nadhani sasa itakuwa ngoma droo. Mwenye chuki atajulikana,” alisema Jome.

***

Pale kwenye meza yao, mama Shua alikuwa akitokwa na jasho, lakini hakuwa na la kufanya. Mapigo ya moyo yalimwenda kwa kasi. Alifikiria nini kitatokea endapo mumewe ataamua kufanya fumanizi hotelini na wateja kibao wakishuhudia…

“Musa nifanyeje?” aliuliza Maua…

“Kwa kweli huna la kufanya, maana unajua hata ukisema uondoke atakuona, ukisema uende uani, atakuona. Yaani wapo hapo nyuma yako,” alisema Musa kwa sauti ya chini sana ili asisikike.

Dakika kumi mbele, Maua aliwasili. Kweli alishuka akiwa kwenye usafiri wa bodaboda, akalipa, akaingia ndani kumfuata baba Shua…

“Sikia mama Shua…sasa kuna dada mmoja ameingia, naona anakuja kukaa nao,” Musa alimwambia mama Shua…

“Kweli? Atakuwa nani? Unaweza kumpiga picha kwa simu nikamwona?”

“Yeah! Ngoja nifanye hivyo…da! Halafu anambusu mume wako…na yeye anambusu pia…sasa anavuta kiti na kukaa jirani na mume wako…” Musa alimpa picha kamili mama Shua huku akimpiga picha…

“Huyu hapa,” alimwonesha mama Shua picha hiyo…

“Haa! Namjua huyu dada, anaitwa Maua. Ndiyo alikuwa amuoe kabla yangu…ina maana baba Shua amerudiana na huyu mwanamke kweli..? Haiwezekani,” alisema akilia mama Shua.

***

“My sweetheart Maua,” aliita baba Shua…

“Yes baby…”

“Unajua kwa nini nimekuita hapa?”

“No! Sijui kama kuna kitu zaidi ya kuamini umependa uwe na mimi muda huu.”

“Hilo ni moja na dogo sana. Ila kubwa ni kwamba, mke mwenzio yule pale. Na yupo na yule kijana niliyekwambia ndiye anayemzuzua.”

“Haa! Benny…”

“Nini Maua?”

“Yaani unashuhudia hayo na unafumbia macho? Au umeshakwenda kuzungumza nao?”

“Hapana shemeji Maua…unajua huyu bwana kwa hali ilipofikia, akisema aanze kufuatilia mpaka kuzungumza au kufumania atavuruga fiucha yake bure, hii ndiyo inatakiwa. Uamuzi ni wake sasa, aamue kuendelea kuwa na mwanamke huyu au aachane naye…wewe si upo bwana,” alidakia Jome, Maua akaachia tabasamu jepesi, hasa baada ya kusikia yeye yupo.

Baba Shua akabakia kumkazia macho Maua kama anayesema moyoni ‘maneno ya Jome ni kweli kabisa.’

“Sawa, lakini sasa mwisho wake ni nini?” aliuliza Maua…

“Dawa ya wale ni kuwaita hapa kisha kukabidhiana. Benny mkabidhi mama Shua kwa yule kijana halafu wewe jikabidhi kwa Maua hapa,” alisema Jome.

“Hapana, mimi ninachotaka ufanya si hicho. Nataka wakati wa kuondoka nikawaage lakini safari yangu breki ya kwanza ni nyumbani, nikachukue nguo zangu niondoke. Sikuwa na lengo la kutengana na yeye, ila kwa tabia yake imebidi. Hata kujitokeza kwa Maua naamini ni Mungu tu kwani kaja wakati mwafaka…

“Kwa mwanaume yeyote yule hawezi kuvumilia ujinga wa huyu mwanamke. Kweli kabisa mke ndani ya nyumba anakwenda kuingia kwenye chumba cha mpangaji mwingine na kufanya usaliti wa wazi? Ningekuwa mtu mwingine ningevunja ule mlango na kuua…”

“Kweli kabisa,” alidakia Jome.

Walikunywa ndani ya nusu saa tu, ukafika muda wa kuondoka. Wakasimama wote, wote wakaenda kwenye meza ya akina mama Shua…

“Jamani tumechelewa kuwasalimia lakini kwa sababu tunaondoka acha tuwape hai,” alisema baba Shua huku akiwapa mkono akianzia na Musa.

“Poapoa,” alijibu Musa kwa kujikaza sana. Mama Shua aliinama kwa aibu…

“Za leo?” Maua alimsalimia Musa tu, akaondoka.

Jome yeye hakusalimia yeyote yule, naye akafuata nyuma ya Maua. Baba Shua akafuatia, wakaingia kwenye gari na kuondoka.

***

“Musa,” aliita mama Shua…

“Vipi?”

Leave A Reply