The House of Favourite Newspapers

Cioaba na Dube Wapeta Mwezi Septemba

0

ARISTICA Cioaba, Kocha Mkuu wa Azam FC ameteuliwa kuwa Kocha Bora wa Ligi Kuu Bara mwezi Septemba pamoja na mshambuliaji wake namba moja ndani ya Azam FC na Ligi Kuu Bara, Prince Dube.

 

Cioaba aliwashinda makocha wawili ambao ni Sven Vandenbroeck wa Simba ambaye kwenye mechi nne alipata sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Mtibwa Sugar na alishinda tatu na Zlatko Krmpotic wa Yanga alipata sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Tanzania Prisons na alishinda tatu kwa mujibu wa Kamati ya Tuzo ya VPL inayotolewa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Septemba, Cioaba alishinda michezo minne na kukusanya pointi 12 huku wachezaji wake wakifunga mabao manne ilikuwa namna hii:- Azam 1-0 Polisi Tanzania, Azam 2-0 Coastal, Mbeya City 0-1 Azam na Prisons 0-1 Azam FC.

 

Kwa upande wa Dube, alitwaa tuzo hiyo akiwashinda David Kissu wa Azam FC ambaye yeye ni kipa hakufungwa bao kwenye mechi nne na kiungo wa Simba, Clatous Chama ambaye alifunga mabao mawili na kutoa pasi moja.

Dube alifunga mabao matatu na kutoa pasi moja ya bao kwenye mechi nne za ligi ambapo alianza kutoa pasi kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya Polisi Tanzania, alifunga mbele ya Coastal Union mabao mawili na bao lake la tatu alifunga dhidi ya Tanzania Prisons. Kwa sasa ni kinara akiwa na mabao matano na jumla ana pasi mbili za mabao.

STORI NA LUNYAMADZO MLYUKA, Dar es Salaam

Leave A Reply