The House of Favourite Newspapers

Clinton: Naweza Kumteua Obama Kuwa Jaji Mahakama Kuu

0

WASHINGTON, DC - APRIL 22:  Democratic presidential candidate and former U.S. Secretary of State Hillary Clinton delivers remarks at the Hillary Rodham Clinton Awards for Advancing Women in Peace and Security at Georgetown University April 22, 2015 in Washington, DC. The awards were given to former United Nations Envoy for Afghanistan Staffan de Mistura, and Dr. Miriam Coronel-Ferrer, who served as the Chief Negotiator of the Philippines Government in the Mindanao Peace Talks.  (Photo by Win McNamee/Getty Images)Bi. Hillary Clinton

Mgombea urais wa Marekani kwa tiketi ya Chama cha Democratic, Bi. Hillary Clinton amesema endapo ataingia madarakani, linaweza kuwa wazo zuri sana kumteua Rais wa sasa wa nchi hiyo, Barack Obama kuwa Jaji wa Mahakama Kuu nchini humo.
Bi. Hillary Clinton ameyasema hayo alipokuwa akijibu swali aliloulizwa na mpiga kura katika mkutano wa kampeni uliohudhuriwa na watu takribani 450 Jimbo la Iowa, ambapo raia hyo alimtaka  Clinton aeleze iwapo baada ya kuwa rais wa nchi hiyo, anaweza kufikiria kumteua rais Obama kuwa Jaji wa Mahakama Kuu kwa sheria za nchi ya Marekani zinaruhusu rais atakayeingia madarakani ana kuteua majaji watatu wa Mahakama Kuu, shirika la habari la ABC News limeripoti.

Barack ObamaRais Barack Obama

“Lo! Hilo ni wazo zuri sana. Hakuna mtu amewahi kupendekeza hilo kwangu,” alisema Bi. Clinton.
“Nalipenda sana wazo hilo. Anaweza kuwa na mambo mengine kadha ya kufanya, lakini nakwambia hilo ni wazo zuri sana.”
“Ni mwerevu sana, na anaweza kutetea hoja vyema, na alikuwa profesa wa sheria, kwa hivyo amehitimu,” alisema.

“Sasa, tunahitaji kuwa na Bunge la Seneti linalodhibitiwa na Chama cha Democratic ndipo aweze kuidhinishwa, kwa hivyo mtanisaidia kufanya hilo, tumekubaliana?”

Bi Clinton, alishindana vikali na Obama kuwania tiketi ya kupeperusha bendera ya urais mwaka 2008 lakini akashindwa na baadaye Obama alipoingia madarakani akamteua kuwa Waziri wa Mashauri ya Kigeni.

Leave A Reply