The House of Favourite Newspapers

Coastal Union Yamganda Ali Kiba

UONGOZI wa Coastal Union umesema kuwa kuelekea msimu ujao hawana mpango wa kumuacha mchezaji wao Ali Kiba kwa kuwa wameridhika na uwezo wake licha ya kubanwa na majukumu yake.

 

Kiba ambaye alisajiliwa msimu huu na Coastal Union alicheza mchezo mmoja kwenye ligi dhidi ya Mbeya City huku ule dhidi ya Kagera Sugar akifanyiwa mabadiliko dakika za lala salama.

 

Akizungumza na SpotiXtra, Kocha Mkuu wa Caostal Union, Juma Mgunda alisema kuwa malengo yao makubwa ilikuwa ni kuunda kikosi kitakachokuwa na muunganiko mzuri msimu ujao hivyo hawana hesabu za kuwaacha wachezaji wake tegemeo.

 

“Wachezaji wetu ambao tumeanza nao baada ya kupanda daraja ni lazima tubaki nao kwani wengi tumeanza nao mbali, hata huyu Ali Kiba nina imani tutakaa naye chini tena kuzungumza kwani licha ya kubanwa na ratiba bado amekuwa na mchango kwenye kikosi.

 

“Mwalimu mzuri anawajua wachezaji sasa Kiba siwezi kumuacha msimu ujao jina lake lazima niwe nalo kwa kuwa kwa sasa tuna uhakika wa kubaki ligi kuu tunachokifanya ni kuangalia sehemu ambazo zimekuwa na mapungufu ili tufanyie maboresho,” amesema Mgunda.

 

Coastal Union ipo nafasi ya 10 baada ya kucheza michezo 37 na imejikusanyia jumla ya pointi 37 mchezo wake wa mwisho msimu huu utakuwa dhidi ya Singida United uwanja wa Mkwakwani.

Comments are closed.