The House of Favourite Newspapers

Coca-cola Yaitambulisha ‘Sisimua Maisha na Fanta’

0
Meneja Masoko wa Kampuni ya Coca-Cola Tanzania, Kabula Nshimo (kulia) na Meneja Mauzo wa Coca-Cola Kwanza, Fredrick Mtui wakifurahia jambo wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kampeni ya ‘Sisimua Maisha na Fanta’.

Kampuni ya Coca Cola Tanzania, imezindua kampeni ya Sisimua Maisha na Fanta katika hafla iliyopambwa na burudani mbalimbali jijini Dar es Salaam.

 

Mtangazaji wa kipindi cha Genge cha E-fm al-maarufu ‘Fido’ (kushoto) na Mtangazaji wa East Africa Radio, ‘DullahPlanet’ wakiwa katika picha ya pamoja.

 

Katika uzinduzi huo, wapenzi wa kinywaji hicho, walipata fursa ya kushiriki burudani na michezo mbalimbali kabla ya kuingia kwenye treni linalofanya safari kati ya Ubungo na Stesheni ambalo lilikua na chapa na rangi mbalimbali za Fanta.

 

Mtangazaji wa East Africa TV, Kelvin Lyimo ‘Kevoo’ (kulia) akifurahia picha ya pamoja na wanafunzi wa Sekondari wa jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kampeni ya ‘Sisimua Maisha na Fanta’.

 

Kabula Nshimo ambaye ni Meneja Masoko wa Cocacola Tanzania, amesema lengo la kuzindua kampeni ya Sisimua Maisha na Fanta ni kuwaleta pamoja wapenzi wa kinywaji hicho na kuwahamasisha watu wengine kuendelea kunywa soda hiyo maarufu lakini pia kuwahamasisha kushiriki kwenye michezo na burudani mbalimbali kila wanapopata nafasi.

Mtangazaji wa vipindi vya Televesheni Salama Jabir, Winnie Nzunda na Rukia Yazid wakishiriki kwenye baadhi ya michezo iliyofanyika wakati wa hafla hiyo.

 

Wapenzi wa soda ya Fanta jijini Dar es Salaam wakifurahia uzinduzi wa Kampeni ya ‘Sisimua Maisha na Fanta’ ndani ya treni la abiria.

 

Mtangazaji wa kituo cha redio cha E-fm, Hamis Mandi ‘B-Dozen’ akifurahia jambo na marafiki wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kampeni ya ‘Sisimua Maisha na Fanta’.

 

Mshereheshaji Japhet Mwaipopo akiuliza maswali kwa wageni waalikwa wakati wa hafla hiyo.

 

Na Mwandishi Wetu

Leave A Reply