Coco Beach Yafungwa

MEYA wa Kinondoni, Benjamin Sitta,  ametangaza rasmi kufungwa kwa ufukwe wa Coco Beach kwa miezi Sita ili kupisha ujenzi wa ufukwe huo kwa ukubwa wa kilomita tano ili kuuendeleza, ambapo tayari manispaa imemkabidhi mkandarasi eneo husika kwa ajili ya ujenzi.

 

Mradi huo utagharimu Sh. bilioni 13.6. Kufuatia ujenzi huo,  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kinondoni, Aron Kagurumjuli,  aliongeza kusema kuwa ufukwe wa Coco Beach, umefungwa kwa wafanyabiashara, wakiwemo wauza mihogo wanaotakiwa kutafuta fukwe nyingine.


Loading...

Toa comment