Kartra

Colombia Mshindi wa Tatu Copa America

MCHEZO wa kumtafuta mshindi wa tatu wa Michuano ya Copa America 2021 uliopigwa kwenye Uwanja Estadio Nacional de Brasilia nchini Brazil, usiku wa kuamkia leo, umeshuhudia Colombia wakiibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Peru na kuibuka washindi wa tatu, na hii ni mara ya tano kwenye historia ya Copa America.

 

Fainali ya Copa America itapigwa usiku wa leo saa tisa kamili kwenye Dimba la Maracana ambapo Neymar na Messi watakuwa na kibarua kizito cha kuongoza timu zao pale Brazil wakimenyana na Argentina.

 


Toa comment