The House of Favourite Newspapers

Comedian Zelensky Ashinda Urais

Mchekeshaji wa Ukraine, Volodymyr Zelensky amepata ushindi mkubwa katika uchaguzi wa urais baada ya kumshinda mpinzani wake, Petro Poroshenko, ambaye ndiye rais aliyekuwa madarakani.

Mchekeshaji huyo asiye na uzoefu wa kisiasa ameshinda kwa kishindo katika uchaguzi wa rais nchini Ukraine jana, na kupongezwa na viongozi mbalimbali  duniani.

Bwana Zelensky mwenye umri wa miaka 41, ameweza kumtoa madarakani rais Poroshenko ambaye amekubaliana na matokeo hayo.

Zelensky amekuwa akicheza mchezo wa kuigiza unaoitwa ‘Servant of the People ‘ ambapo amekuwa akiigiza kama kiongozi  anayetaka kuwa rais wa Ukraine.

Mchekeshaji huyo ameshinda kwa kunyakua asilimia 73 ya kura zote zilizopigwa, huku Poroshenko amepata asilimia 24 tu ya kura hizo lakini matokeo rasmi bado hayajatangazwa.

Kampeni za urais za Zelensky hazikuwa na mihadhara ya kijadi, badala yake mchekeshaji huyo alikuwa na hafla za vichekesho, pamoja na kuwavutia wapiga kura kupitia mitandao ya kijamii.

Comments are closed.