Corona: Bodaboda Aliyeuawa Alimpeleka Mjamzito Hospitali

Familia moja nchini Kenya yataka haki itendeke baada ya kifo cha Khamisi Juma Bega (49), bodaboda ambaye alipigwa na polisi hadi kufa.

 

Inadaiwa Khamisi alipigwa na maafisa wa polisi wakishinikiza kufuatwa kwa sheria ya kubaki ndanii kwa kipindi hiki chenye tishio la #Covid19.

 

Ijumaa, siku ya kwanza ya zuio la kutoka nje, Khamisi alipigiwa simu na mteja wake mjamzito, aliyetarajia kujifungua hivi karibuni. Mjamzito huyo alimuomba Khamisi ampeleke hospitali, ambako alikutwa na mkasa huo.

 

Ilikuwa ni majira ya saa moja na nusu usiku alipokuwa akirudi kutoka hospitali, alikutana na maaskri waliokuwa kwenye doria. Inasemekana alipigwa na hakuweza kupatiwa matibabu kwa usiku huo na alipaswa kutulia hata kesho yake, Khamisi alifariki kutokana na majeraha hayo.

 

Polisi wamekataa madai hayo, kamanda wa Polisi Francis Mguli amesema watachunguza tukio hilo. Wakazi wameomba IGP awaatahadharisha polisi kwenye kutumia nguvu katika kutekeleza agizo.

Toa comment