The House of Favourite Newspapers
gunners X

Corona: China Kujenga Hospitali Siku 6 Kuokoa Waathirika

0

MJI wa Wuhan nchini China unaharakisha kujenga hospitali mpya kusaidia kutibu wagonjwa waliokumbwa na virusi vya Corona ambavyo vimeshaua watu 80 na zaidi ya 870 wameambukizwa nchini humo.

 

Kusambaa kwa virusi hivyo kulianzia kwenye mji huo ambapo sasa madaktari wanasema waathirika wanapanga foleni kwa muda mrefu wakiwa kusubiri huduma. Uzuiaji wa ugonjwa huo unakuwa mgumu kutokana na uchache wa vifaa vya kujilinda na baadhi ya madaktari kuambiwa wasiende kutoa huduma wakihofiwa kupata maambukizi.

Mamlaka katika mji wa Wuhan zinasema hospitali hiyo inatarajiwa kuwa na uwezo wa kuweka vitanda 1,000 vya wagonjwa na inatarajiwa kuanza kutumika Februari 03, mwaka huu.

 

Mwaka 2003, Beijing ilijenga Hospitali ya Xiaotangshan ndani ya siku saba iliyosaidia kutibu waliougua SARS (Severe Acute Respiratory Syndrome), ugonjwa ulisababishwa na virusi pia na kuua takriban watu 774 Duniani kwa mwaka 2002 na 2003.

 

Kamisheni ya Afya ya Taifa la China imesema, kasi ya maambukizi ya kirusi  Corona inaelezwa inaweza kuongezeka sana na kuna uwezekano idadi ya wagonjwa ikaongezeka pia. Mpaka sasa watu zaidi ya 2,000 wameshaambukizwa funiani na watu 56 wameshapoteza maisha kutokana na ugonjwa huo.

Kirusi hiki kinaaminika kilianza katika Soko la Bidhaa za Baharini mwishoni mwaka 2019, katikati ya Jiji la Wuhan, China, ambalo lilikuwa linauza nyama ya porini na kimeenea katika miji mingine ikiwemo Beijing na Shanghai, Marekani, Thailand, Korea Kusini, Japan, Australia, Ufaransa, na Canada.

 

Jana Jumapili, China ilitangaza Katazo la Kuuza Nyama ya Porini katika masoko, migahawa na mitandao ya kieletroniki ya biashara nchini kote.

Leave A Reply