JESHI la Polisi nchini Kenya linawasaka watu 50 waliotoroka katika kituo cha Kenya Medical Training College, mjini Nairobi kilichokuwa kinatumika kama karantini kwa waathirika walioambukizwa virusi vya corona na wenye dalili za covid – 19.
Inadaiwa kuwa walikuwa wanapata chakula cha jioni, na mvua ilikuwa inanyesha hivyo wakatumia fursa hiyo kuruka uzio na kukimbia.
Wengine kati ya hao waliotoroka walikuwa wanasubiri majibu ya vipimo vyao kama wana #CoronaVirus, huku walikuwa katika uangalizi kama wangeonyesha dalili yoyote ya kuwa na virusi hivyo.
Hadi hivi sasa Kenya ina jumla ya visa 296 vya #Covid19. Huku watu 92 wakiwa wamekamatwa na watawekwa karantini kilazima baada ya kukiuka sheria ya kuachia mita moja.