RAIS wa Uganda, Yoweri Museveni amewaonya wananchi wanaoenda kinyume na taratibu wakati huu wa vita dhidi ya #CoronaVirus.
Museveni amesema Mungu yuko bize, ana kazi nyingi, hawezi kuwa Uganda akiwaangalia wajinga, ameongeza kwamba Uganda imepewa taarifa za kutosha ili kujilinda na Covid-19, hivyo kama watu hawafuati maelekezo, Mungu na serikali hawawezi kulaumiwa.
Ameongeza kuwa Mungu amewalinda na hakuna kifo mpaka sasa, lakini anahitaji kuwaangalia watu wengine walio katika wakati mgumu.


