The House of Favourite Newspapers

Corona: Raia Wapigwa Risasi kwa Kukiuka Agizo la Rais

0

WATU wawili wamelazwa hospitali nchini Uganda baada ya kupigwa risasi na polisi kwa kukiuka agizo la Rais Yoweri Museveni la kupiga marufuku bodaboda.  Watu hao, Alex Olyem na Kasim Ssebude, wamepigwa risasi wakiwa wamepakizana kwenye bodaboda ambazo zimepigwa marufuku ili kuzuia corona kuenea.  Mmoja amepigwa tumboni na mwingine mguuni.

 

“Alex na Kasim wamepigwa risasi kwa kubishana na askari, wanadai hawakusikia  kwenye vyombo vya kuhusu kupigea marufuku kwa  bodaboda kupakiza abiria.  Mwanzoni risasi zilipigwa juu wakawa wanakimbia, zikapigwa tena mmoja ikampata mguuni mwingine tumboni.  Wamelazwa,” imesema Polisi nchini Uganda.

Aidha, Polisi Uganda wamekamata Bodaboda 500 na Taxi takribani 170 hadi sasa kufuatia baadhi ya Watu kikiuka maagizo ya Rais Museveni ya kupiga marufuku usafiri wa umma kwa siku 14, Watu 10 wamekamatwa pia kufuatia kubishia maagizo ya Polisi, stendi zimefungwa.

 

Leave A Reply