The House of Favourite Newspapers

Corona: Rais DRC Atangaza Hali ya Hatari Nchi Nzima

0

RAIS Felix Tshisekedi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ametangaza hali ya hatari nchini kote, ikiwa ni juhudi za kupambana na virusi vya Corona.

 

Amesema, uamuzi huo umetokana na hatari kubwa ya virusi hivyo, na kutangaza hatua nyingine kadhaa ikiwemo kusimamisha safari zote za kuingia na kutoka katika mji mkuu wa Kinshasa na mikoa mingine ili kuuweka mji huo kwenye karantini.

 

Ameitaka  polisi na vikosi vya usalama kufanya doria ya pamoja ili kuhakikisha hatua hizo zinatekelezwa kwa manufaa ya watu wote.

 

Pia ametangaza kufunga mipaka na kuruhusu malori, meli na ndege za mizigo muhimu tu kuingia nchini humo. Mpaka sasa, kuna jumla ya kesi 48 za maambukizi ya virusi vya Corona nchini humo.

 

Leave A Reply