DUNIA nzima inatetemeka, janga la covid 19 linatishia maisha ya kila mmoja wetu, watu wamejifungia ndani, Siyo Amerika, Ulaya, Asia wala Afrika, kila mmoja analia kilio chake, uchumi unatetereka. Si matajiri wala maskini, ugonjwa huu unakumba yeyote.
Mlipuko wa Homa hii ya mapafu inayosababishwa na virus vya CORONA, ambayo ilianzia China na kusambaa katika mataifa mengine duniani, mpaka sasa ugonjwa huu mesababisha vifo vya maelfu ya watu duniani kote kutokana na kasi kubwa ya maambukizi hayo ikizingatiwa kwamba ugonjwa huu haujapa kinga wala tiba.
Kwa akili zao, elimu zao, maarifa na upeo wao wote, wataalamu wa afya wanaendelea kuhangaika kutafuta chanzo, kinga na tiba Corona, lakini kwa sasa wanatibu dalili pekee.


