The House of Favourite Newspapers

Corona: Wageni Waongezewa Muda Kukaa Tanzania

0

KUTOKANA  na mlipuko wa ugonjwa unaosababishwa na virusi vya Corona  — #Covid-19 — na baadhi ya wasafiri kushindwa kusafiri kurudi kwao, Tanzania imetoa muda wa nyongeza kwa wageni hao kukaa nchini.

Wageni wote waliokuwa wanatarajia kuja na tayari wamepewa ‘Visa Grant Notice’ lakini wameshindwa kusafiri wameongezewa miezi mitatu kutoka muda wa visa zao ulipoanza.

Wageni ambao pasi zao za kusafiria zimeisha muda au zinakaribia kuisha muda na hawawezi kusafiri kutokana na mlipuko wa ugonjwa huo, wanatakiwa kwenda kituo  chochote cha karibu cha uhamiaji ili kuongezewa mwezi mmoja wa bure kwenye pasi zao za kusafiria.

Hata hivyo,  kama hali hii itaendelea baada ya kuisha kwa mwezi mmoja wa nyongeza, wageni hao watatakiwa kufika katika Ofisi za Makao Makuu ya Uhamiaji yaliyopo Kurasini, Dar es Salaam.

Kwa wale wenye kibali cha ukazi, pasi ya kusafiri ya wageni (Exemption Certificate) na ‘Dependant Pass’ ambazo zimeisha muda, wamepewa mwezi mmoja wa nyongeza kukaa nchini. Lakini muda huo ukikaribia kuisha wanashauriwa kufika Makao Makuu ya Uhamiaji.

Aidha, wale wote wenye kibali au pasi ya ukazi ambao tayari wameshakusanya nyaraka zao, wanatakiwa kuripoti mara moja Makao Makuu ya Uhamiaji yaliyopo Kurasini Dar es Salaam.

Leave A Reply