The House of Favourite Newspapers

Cosmas Cheka na Suma Ninja Kutwangana Laivu Mkesha wa Mwaka Mpya

0

29 Desemba 2022: BONDIA Cosmas Cheka kutoka mkoani Morogoro anatarajiwa kuzinyuka na Suma Ninja mwenye maskani yake jijini Dar katika pambano litakalofanyika mkesha wa mwaka mpya 2023 katika Ukumbi wa Green City uliopo Makambano mkoani Njombe.

Akizungumza na Global Publishers, muandaaji wa pambano hilo, bondia mkongwe, Omary Yazidu na Kampuni ya Kas Promotion amesema kabla ya pambano hilo kutakuwa na mapambano mengine 12 ya utangulizi.

Yazidu amesema maandalizi yote ya mpambano huo yameshakamilika na kinachosubiriwa ni saa na muda wa kupanda uliongoni hivyo anawakaribisha wapenzi wa burudani kufika wajishuhudie wenyewe ndonga za kufa mtu.

Muandaaji huyo alitumia nafasi hiyo kuwashukuru wadhamini waliomsaidia kufanikisha maandalizi hayo wakiwemo Kihwelo Safari, Kihwelo Mobile Money, Mc Mwendokasi na wengineo.

Leave A Reply