Country Wizzy Akiri Kumuiga Lil Wayne
GUMZO lililozungu mzwa siku chache zilizopita, lilikuwa ni usajili wa Ibrahim Mandingo ’Country Wizzy’ ambaye ametua pale kwenye lebo ya staa wa Bongo Fleva, Rajabu Abdul ‘Harmonize’.
Kabla ya kutua kwenye lebo hiyo, Country hakuwa mchanga kwenye gemu, kwani tayari alishaachia mikwaju mikali ikiwemo Yule Boy, Watoto, Watakoma, Wanaona Haya, Leo, Turn Up na nyingine kibao!
MIKITO NUSUNUSUimefanya naye mahojiano, mara baada ya kujiunga na lebo hiyo, ambayo inamilikiwa na Harmonize au Harmo ambaye ni staa wa Bongo Fleva, kwa sasa anajulikana zaidi kwa jina la Country Wizzy na si Country Boy, kama alivyokuwa akifahamika zamani;
MIKITO: Hongera kwa kazi nzuri ambayo unaendelea kufanya kwenye muziki wako.
COUNTRY WIZZY: Ahsante sana.
MIKITO: Hebu wakumbushe mashabiki, umeanza kazi ya muziki lini?
COUNTRY WIZZY: Mimi nilianza muziki tangu mwaka 2005, na nilikuwa nimesajiliwa Baucha Records, lakini kutokana na mambo ya shule, ilibidi ni-stop kwanza ili nisome.Niliendelea na elimu yangu ya sekondari mpaka mwaka 2017 nikaingia chuo, nilipomaliza chuo 2010, ndipo nikaanza rasmi muziki na ngoma yangu ya kwanza inaitwa Your The One.
MIKITO: Ni msanii gani ambaye aliweza kukuvutia hadi ukaamua kuingia kwenye muziki?
COUNTRY WIZZY:Hakuna msanii ambaye nilikuwa namtamani kama marehemu Albart Mangwea, yaani nilikuwa napenda kusikiliza sana ngoma zake.
MIKITO: Mashabiki wanasema kwamba, unamuiga sana Lil Wayne, staa wa Hip Hop Marekani. Je, kuna ukweli wowote?
COUNTRY WIZZY:Ni kweli kwa sababu ni msanii ambaye nampenda toka enzi hizo kwa sababu ana swaga ambazo mimi napenda, ni role model wangu. Ndiyo maana unaona kuna vitu ambavyo tunafanana, pia hapa nilipo natamani kuwa kama yeye.
MIKITO: Ni muziki gani ambao ulikutambulisha rasmi kwenye tasnia?
COUNTRY WIZZY: Ni ngoma ambayo nilifanya na Linah, inaitwa Mateso, ni wimbo ambao ulifanya poa sana na kila mtu alipenda ujumbe ambao ulikuwa ndani yake.
MIKITO: Kwa upande wako, unamzungumziaje Harmonize kama bosi wako mpya?
COUNTRY WIZZY:Ni mtu ambaye ana upendo sana, anajituma, yaani angekuwa msanii mwingine kwa level ambayo amefikia, angejihisi amemaliza lakini Harmo bado anapambana kuhakikisha kila mwenye hitaji anafanikiwa. Anatamani kufikisha muziki wetu mbali zaidi ya hapa.
MIKITO: Kuna maneno yanayosambaa kwenye mitandao kuwa, Harmonize kakupendelea, labda tungependa kufahamu wewe na Harmonize mna muda gani tangu mjuane?
COUNTRY WIZZY: Mimi na Harmo tuna mwaka wa tatu sasa.
MIKITO: Wewe ni msanii mkubwa halafu umesajiliwa na Harmo, huoni kama itatokea kama yale ya Rich Mavoko kwamba akajikuta ameshindwa ku-shine aliposajiliwa
WCB?COUNTRY WIZZY:Kwa kweli sijajua, mimi nadhani kwa upande wangu ninachoweza kuangalia yanayonihusu, na kabla ya kufanya kazi hapa, mimi nilishakuwa kama mwanafamilia na pia naomba Mungu sana yasije yakatokea mabaya dhidi yetu.
MIKITO: Kuna EP (Extended Playlist) ya The Father, unaiyachia lini?
COUNTRY WIZZY:Tarehe 25 mwezi huu, ndiyo naiachia.
MIKITO: Ina jumla ya nyimbo ngapi?
COUNTRY WIZZY: Ina nyimbo saba.MIKITO: Imezoeleka kwamba EP huwa ina jumla ya ngoma tatu hadi nne, ila kwako kuna ngoma saba ambayo ni sawa na Album kabisa. Kwa nini umeamua kufanya hivyo?
COUNTRY WIZZY:Kweli ni ngoma nyingi kwa EP, ila ninachokitaka ni watu waburudike, lakini pia nimepata nafasi ya kusajiliwa kwenye lebo kubwa, sasa kwa nini nisifanye mambo makubwa?
MIKITO: Kwenye EP yako, umewashirikisha wasanii wa aina gani?
COUNTRY WIZZY:Nimemshirikisha msanii mwenzetu wa hapa Konde Gang, Skales kutoka Nigeria, Konde Boy na wasanii wengine kutoka South Afrika, yaani kuna ‘koloboresheni’ kama nne kwenye EP yangu.
MIKITO: Matarajio yako yapo vipi hapo Konde Gang, unajiona nani baadaye?
COUNTRY WIZZY:Matarajio ni makubwa sana, pia najiona kama msanii mkubwa sana hapo mbeleni.
MIKITO: Asante kwa muda wako.
COUNTRY WIZZY:Shukran pia.
MAKALA: KHADIJA BAKARI