The House of Favourite Newspapers

Coutinho awekwa sokoni

0

TINYO

Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Mbrazili, Andrey Coutinho.

Khadija Mngwai na Said Ally
MAISHA ya kiungo mshambuliaji wa Yanga, Mbrazili, Andrey Coutinho, ndani ya kikosi hicho kwa sasa yanaweza kuwa mafupi kufuatia uongozi wa klabu hiyo kumuweka katika hesabu za kumpiga bei endapo watapata ofa nzuri kutoka kwa timu yoyote ile.

Coutinho ambaye aliletwa nchini na aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Mbrazili, Marcio Maximo, kwa sasa hana nafasi katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo ambapo mara kwa mara amekaririwa akilalamikia hali ya kupigwa benchi.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Katibu wa Yanga, Dk Jonas Tiboroha, alisema klabu hiyo ipo tayari kumuuza Mbrazili huyo ambaye alipoingia kama mchezaji wa akiba katika mchezo dhidi ya Toto wiki iliyopita, alionyesha kiwango kikubwa, akiwa anacheza kwenye ligi kuu kwa mara ya kwanza msimu huu.

“Tupo tayari kumuuza Coutinho iwapo itatokea dau lolote kubwa na tutamuacha aende, lakini hatuna mpango wa kumuacha kwenye dirisha dogo, tupo tayari kumuuza mchezaji yeyote yule kwa kuangalia dau kubwa.

“Lakini tutafanya hivyo endapo kama itatokea timu yoyote ile ambayo itakuwa tayari kukubaliana na sisi juu ya bei ya kumuuza kiungo huyo na tukishaafikiana, hatutakuwa na sababu ya kumzuia kuendelea kuwepo ndani ya kikosi chetu,” alisema Tiboroha ambaye ni mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Leave A Reply