The House of Favourite Newspapers

CPA Makalla Apanga Mstari Kujiandikisha Katika Daftari la Mkaazi la Uchaguzi Serikali za Mitaa

Katibu wa NEC-Itikadi Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa CPA Amos Makalla ameshiriki zoezi la kujiandikisha kwenye daftari la wakaazi kwaajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwenye Ofisi ya Serikali za Mitaa TPDC Kata ya Mikocheni Wilaya ya Kinondoni Jijini  Dar es salam leo Oktoba 16, 2024.
Akizungumza na wakazi wa Mtaa wa TPDC Mikocheni mara baada ya kujiandikisha CPA Makalla amesema zoezi la kujiandikisha katika daftari la kupiga kura ni muhimu sana na amefurahi kutimiza haki yake ya msingi ya kujiandikisha na amesisitiza kuwa ameridhishwa na utaratibu wa zoezi hilo.
Aidha Makala amewataka Watanzania bila kujali tofauti za kiitikadi kujitokeza kwenye zoezi hilo kwani ni muhimu katika kuweka msingi wa maendeleo ya wananchi.