The House of Favourite Newspapers

CPA. Makalla ” CCM Haiwezi Kujitenga na Matatizo ya Wananchi”

0
Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha mapinduzi (CCM) komredi Amos Makalla, amesisitiza kwamba Chama hicho hakiwezi kujitenga na Matatizo ya Wananchi, hivyo amewataka watendaji wa Serikali wakiwemo Wakuu wa Mikoa, Wilaya na Wakurugenzi kuendelea na Utaratibu wa kutenga muda ili Kusikiliza na Kutatua kero mbalimbali za Wananchi.
CPA. Amos Gabriel Makalla ambaye ameteuliwa na Mwenyekiti wa CCM Rais Samia Suluhu Hassan kuwa mlezi wa CCM mkoa Dar es Salaam ametoa kauli hiyo leo Julai 06, 2024 katika ukumbi Diamond Jubelee jijini humo,wakati akizungumza na Wana CCM waliofika kwenye mapokezi yake, ikiwa ni Siku ya kwanza ya Ziara yake ya Siku 7 ndani ya mkoa wa Dar es Salaam.
Leave A Reply