The House of Favourite Newspapers

CPA Makalla: Lissu na Wenzake Hawana Mamlaka ya Kuzuia Uchaguzi

KATIBU wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapunduzi (CCM),CPA Amos Makala amewataka Watanzania kupuuza madai ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwamba uchaguzi hautafanyika bila mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi.

Akizungumza  katika mkutano wa viongozi wa chama na jumuiya ngazi ya shina, tawi, kata na wilaya katika Wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es salaam CPA, Makalla amesema kuwa CHADEMA inafanya Makosa kuwahadaa wananchi  wasijiandikishe kwa madai kuwa hakutakuwa na uchaguzi.

Amesisitiza kuwa uchaguzi utafanyika kwa mujibu wa sheria na katiba, na kwamba madai ya CHADEMA kwamba “No Reform, No Election” ni propaganda zisizo na msingi na hivyo zipuuzwe.

Vilevile amewataka wenyeviti wa serikali za mitaa waliochaguliwa katika uchaguzi uliofanyika Novemba Mwaka jana kutanguliza huduma na utumishi kwa wananchi wao, kwani waliomba utumishi na wawakiwakilishe chama kama walivyoaminiwa.