The House of Favourite Newspapers

CRISTIANO RONALDO APIGWA FAINI YA SH. BILIONI 49

 

MSHAMBULIAJI  wa Klabu ya Juventus, Cristiano Ronaldo, amekubali kulipa faini ya Euro milioni 18.8 sawa na shilingi bilioni 49.3 za Tanzania kwa kosa la ukwepaji kodi nchini Hispania.

Kwa mujibu wa hukumu iliyotolewa leo na Mahakama ya Madrid, Ronaldo amekubali pia kifungo cha miaka miwili ambacho hata hivyo hatakitumikia gerezani kutokana na utaratibu wa adhabu za vifungo nchini humo.

Nchini Hispania hukumu ya kifungo kisichozidi miaka miwili hakipaswi kutumikiwa ndani ya gereza isipokuwa kwa kosa la uhalifu.

Ronaldo ambaye ni mshindi mara tano wa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Dunia,  alikuwa akituhumiwa kukwepa kodi kiasi cha Euro milioni 22.4 (Shilingi Bilioni 58.7) kupitia mapato yaliyotokana na matumizi ya picha zake kwenye matangazo mbalimbali kati ya mwaka 2010 na 2014 wakati akiitumikia Real Madrid.

Comments are closed.