The House of Favourite Newspapers

Cristiano Ronaldo Awapaisha Juventus Instagram

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Ureno na Klabu ya Juventus ya Italia, Cristiano Ronaldo, amekuwa kivutio kwa timu yake huku akiiongezea wafuasi milioni 20 Instagram baada ya kuikacha timu yake ya zamani, Real Madrid.

Kabla ya ujio wa mshambuliaji huyo timu hiyo ilikuwa na wafuasi milioni 10 Instagram na kwa sasa imefikisha wafuasi milioni 31 na kuwa kati ya klabu tano duniani zenye wafuasi wengi Instagram.

Timu zenye wafuasi wengi Instagram ni:

1. Real Madrid –  wafuasi milioni 77.6

2. Barcelona – mil. 76.4

3. Juventus – mil. 31.1

4. Manchester United – mil. 31

5. PSG – mil. 23.8

Wafuasi wa Instagram wamekuwa wakidai kupitia mtandao wa kijamii kuwa mvuto wa timu hiyo umeongezeka zaidi baada ya kuwasajili wachezaji wanane wenye viwango vya juu ambao ni Matthijs de Ligt, Danilo, Cristian Romero, Luca Pellegrini, Merih Demiral, Adrien Rabiot, Aaron Ramsey na Gianluigi.

Comments are closed.