Cristiano Ronaldo Kuivaa Man United

NYOTA wa Juventus, Cristiano Ronaldo ana uwezekano wa kuivaa Manchester United katika Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kudaiwa kuwa kuna uwezekano wa adhabu ya kadi nyekundu aliyopata kutoongezwa.

 

Ronaldo alipewa kadi nyekundu katika mchezo dhidi ya Valencia, na atakosa mchezo ujao dhidi ya Young Boys, Oktoba 2, mwaka huu lakini ikiwa atafungiwa mechi mbili ataukosa mchezo unaofuata dhidi ya Manchester United ambao wapo nao kundi moja.

 

Mara baada ya kupata kadi hiyo kumekuwa na gumzo juu ya uhalali kwa kuwa ilionekana ni kama tukio ambalo halikustahili kadi nyekundu.

 

Inadaiwa Vigogo wa UEFA hawana mpango wa kumwongezea adhabu na sasa ina maana atakuwa huru kuivaa Manchester United, Oktoba 23 kwenye Uwanja wa Old Trafford na pia atacheza kwenye mechi ya marudiano dhidi ya timu hiyo, Novemba 7, mwaka huu.

 

Watalaamu wa UEFA wameangalia video za mechi hiyo iliyochezwa Jumatano iliyopita na kuamua kuwa haikuwa kosa kubwa la kuongeza adhabu.

 

Kulikuwa na nafasi ya Juventus kukata rufaa dhidi ya kadi hiyo iliyotolewa na mwamuzi Felix Brych lakini hawakukata rufaa, badala yake kamati ya maamuzi ya UEFA itatoa tamko Alhamisi ijayo.

Loading...

Toa comment