Cuba Yazindua Chanjo ya Corona
CUBA imesema kuwa dozi tatu za chanjo yake dhidi ya virusi vya corona kwa jina Abdala imethibitishwa kuwa na ufanisi wa 92.28% katika awamu ya tatu ya majaribio yake.
Tangazo hilo limekuja siku kadhaa tu baada ya serikali kusema kuwa chanjo nyingine iliyotengenezwa nchini humo inayoitwa , Soberana 2, ilikuwa na ufanisi wa 62% kwa dozi mbili tu kati ya tatu.
“Kwa kuathiriwa vibaya na janga la corona, wanasayansi wetu, katika Taasisi yaFinlay na kituo cha uhandisi wa Jeni na teknolojia ya kibaiolojia wameweza kupita vikwazo vyote na kutupatia chanjo zenye ufanisi mkubwa ,” Rais Miguel Diaz-Canel aliandika kwenye ujumbe wa Twitter.