The House of Favourite Newspapers

Cyril Ramaphosa Achaguliwa Tena kuwa Rais wa Afrika Kusini

0

Bunge nchini Afrika Kusini limemchagua tena Rais Cyril Ramaphosa kuwa Rais wa nchi kwa muhula mwingine tena baada ya kufanyika kwa Muungano kati ya chama cha ANC na vyama vya Upinzani.

Serikali hiyo mpya itakuwa ya Muungano wa ANC, DA na vyama vingine vidogo vidogo kutoka kambi ya Upinzani.

Rais Cyril Ramaphosa kutoka ANC alipata Asilimia ya kura 40 huku DA wakipata kura asilimia 22 ambapo aliingia Madarakani mwaka wa 2018 akichukua nafasi ya Jacob Zuma.

Muungano huo unakuja baada ya hivi karibuni kuwepo kwa maelewano mabaya na mpasuko ndani ya chama kilichopo Madarakani cha ANC.

JOSHUA PIANO AFUNGUKIA SKENDO ya KUMTELEKEZA MTOTO KISA LISHANGAZI, AMTAJA MKE MTARAJIWA

Leave A Reply