D.light, yazindua huduma zake Mbeya

KAMPUNI inayoongoza katika kutoa huduma za umeme wa jua, D.light, ina zaidi ya watumiaji milioni 100 ulimwengu mzima, leo inatangaza kuzindua huduma zake ambazo zitakuwa zikipatikana Kanda ya kusini mkoani Mbeya.
Mikakati ya kampuni hii ni kuhakikisha ifikapo mwaka 2030, wateja zaidi ya bilioni moja wawe wanatumia bidhaa zao za D.light, kutokana na kupatikana kirahisi na kwa gharama nafuu zaidi.
Wateja wanaweza kupata kwa urahisi nishati ya kwa bei nafuu na ya kuaminika ambayo ni safi kutumia sehemu yoyote na wamaanini kituo kipya cha ofisi za Kanda ya kusini kitarahisisha maisha ya watu wa Mkoa wa Mbeya na sehemu za jirani. “Tuligundua kuwa kuna uhitaji na kuamua kuleta bidhaa zetu katika eneo la Kanda ya kusini na ziweze kupatikana kwa urahisi zaidi,” alisema Lilian Mwalongo, Meneja Biashara Kanda ya Kusini.
“Idadi kubwa ya kaya za Kitanzania katika maeneo ya vijijini hazijaunganishwa na gridi ya taifa, wakati kampuni ambazo zimeunganishwa na gridi ya taifa zinachagua nishati ya jua ya bei nafuu kuendesha baadhi ya vifaa vyake. Kwa njia hii kwa kiasi kikubwa inatupa fursa ya kuhudumia wateja zaidi na bidhaa zetu zenye ubora ambazo zinapatikana kwa gharama nafuu zaidi,” Aliongeza “Wateja wetu wanapenda sana huduma hii. Wanatamani kuwa na nishati safi, ya kuaminika na ya bei nafuu.

Kaya ambazo hazijafikiwa na nishati, mara nyingi ndizo zilizo katika mazingira magumu zaidi katika jamii bila kusahau athari kubwa za matumizi ya mafuta ya taa, watoto wanapaswa kusoma kwa kutumia taa zenye ubora.
Bidhaa za D. light ndani ya nyumba zinaleta mwanga safi na salama, kuwa na umeme wa kuaminika kunasaidia kurahisisha matumizi mbalimbali ikiwemo kuchaji simu, kutumia redio na televisheni.
Kituo hiki cha huduma kinaonyesha kuwa d.light ipo mstari wa mbele katika uvumbuzi na utoaji wa suluhisho la kiteknolojia na kutatua changamoto zake.
Hii inaimarisha msimamo wetu juu ya kuunga mkono juhudi za serikali katika kutoa fursa za ajira kwa Watanzania. Kituo hicho kinatarajiwa kusaidia wateja wetu waliopo maeneo mbalimbali kwa ajili ya kupata huduma na bidhaa za umeme wa jua kwa bei rahisi kutoka D.light.

