The House of Favourite Newspapers

Dabi ya Kariakoo! Mugalu Amjaza Upepo Sven Simba

0

 

KUREJEA uwanjani kwa mshambuliaji Mkongomani, Chris Mugalu, kumempa kiburi Kocha Mkuu wa Simba, Mbelgiji, Sven Vandenbroeck na kutamba kuwa hivi sasa ana uhakika wa kuchagua straika gani wa kumuanzisha katika kikosi chake cha kwanza.

 

Hiyo ni baada ya mshambuliaji huyo juzi kurejea uwanjani na kucheza mchezo wa Ligi Kuu Bara akitokea benchi kuchukua nafasi ya John Bocco wakati timu hiyo ilipocheza dhidi ya Kagera Sugar na kufanikiwa kupata ushindi wa mabao 2-0.

 

Timu hiyo, katika michezo yake miwili ya ligi iliyopita ilicheza bila ya Mugalu na Meddie Kagere kabla ya Bocco kurejea mechi dhidi ya Ruvu Shooting Oktoba 26.

 

Hivyo, leo Sven atakuwa ana uwezo wa kuchagua amuanzishe nani kati ya Bocco na Mugalu au kuwachezesha akiamua kutumia mfumo wa 4-4-2.

 

Akizungumza na Championi Ijumaa, Sven alisema kuwa kurejea kwa Mugalu kutamfanya yeye achague straika yupi halisia wa kucheza namba tisa kati yake na Bocco.

 

Aliongeza kuwa Simba ina wachezaji wengi wenye uwezo wa kufunga mabao, lakini hauwezi kupata uhakika wa matokeo mazuri kutokana na baadhi siyo washambuliaji halisi namba tisa.

 

“Simba ina wachezaji wengi wenye uwezo wa kufunga mabao lakini huwezi kuwa na uhakika wa matokeo bila ya uwepo wa washambuliaji halisia wenye uwezo wa kufunga mabao.

 

“Hivyo kurejea kwa Mugalu kutaimarisha kikosi changu na kuchagua mshambuliaji mmoja wa kumuanzisha katika kikosi cha kwanza kati ya Mugalu na Bocco ambaye yeye ana nafasi ya kuanza.

 

“Katika kuelekea pambano hilo ninawahitaji washambulaiji wangu wote wawe fiti ili tuwe na uhakika wa kuchagua mshambuliaji wa kuanza,” alisema Sven.

Wilbert Molandi, Dar es Salaam

Leave A Reply