The House of Favourite Newspapers

Dada agoma Kylie kuolewa na Tyga

0

attends the Alexander Wang Spring 2016 fashion show during New York Fashion Week at Pier 94 on September 12, 2015 in New York City.

Tyga akiwa na mpenzi wake Kylie Jenner.

KENDALL JENNER ambaye pia ni dada wa staa wa Kipindi cha Keeping Up With The Kardashian, Kylie Jenner ameonesha waziwazi kuwa staa wa Hip Hop anaweza kutoka na kushea mapenzi na mdogo wake huyo lakini si kwa jambo la kumuoa.

Chanzo kinasema kuwa hivi karibuni Tyga, Kylie na Kendall walitoka mtoko wa pamoja kwenda kucheza na kufurahia maisha lakini aliposikia kuwa Tyga anatamka hadharani kuwa lazima amuoe Kylie aliamua kuondoka kabisa eneo hilo.

kendall-jenner-hair-22-500x750Kendall Jenner.

“Kendall anampenda sana mdogo wake. Hana tatizo kwa mdogo wake kutoka kimapenzi na Tyga, hivi karibuni walipotoka kwa pamoja kwenda kuponda raha, Tyga alianza kuongelea habari za kutaka kumuoa Kylie na ndipo Kendall alipokasirika na kuamua kuondoka katika chumba walichokuwepo,” kilisema chanzo.

Kendall pia anaamini kuwa mdogo wake huyo amefumbwa macho na mapenzi (mapenzi ni upofu) hivyo hajui litakalomtokea endapo atakuwa na maamuzi ya kung’ang’ania kuolewa.

Leave A Reply