The House of Favourite Newspapers

Dada wa DIAMOND Kutoka Uingereza “Baba Ana Hali Mbaya Sana!” – Video

IKIWA ni siku chache zilizopita, mwanadada anyedai kuwa ni dada wa Staa wa Muziki Bongo, Diamond Platnumz, aitwaye Zubeda kutua Bongo akitokea Uingereza anakoishi, dada huyo amezungumza mazito na kumtaka Diamond awe karibu na baba yake kwani ni mgonjwa sana.

 

Dada huyo ambaye wakati akiwasili nchini alipokelewa na Baba mzazi wa Diamond, mzee Abdul Juma, amesema hajui kipi kibaya ambacho baba alimkosea Diamond hadi kufika hatua ya kuwa mbali naye na kutomsaidia ilihali ni mgonjwa sana akisumbuliwa na tatizo la miguu kuvimba kwa muda mrefu.

 

Lengo la Dada huyo kuja Tanzania ni kutaka kuonana na mdogo wake Diamond ili wazungumze na ikiwezekana wasuluhishe tofauti yake na baba yake. Akipiga stori na Global TV, Zubeda amemuomba Diamond kukubali kuonana nae kwani Baba yake ana hali mbaya kiafya.

VIDEO: MSIKIE HAPA AKIZUNGUMZA

Comments are closed.