The House of Favourite Newspapers

Dada wa Shilole Asimulia Alivyoteseka Kuolewa na Harmorapa

0

DADA wa msanii Shilole ambaye amejitambulisha kwa jina la Khadija Ziota ameeleza kuwa amepitia wakati mgumu na kuteseka wakati anataka kuolewa na msanii Harmorapa kwani mwanzo alikuwa anamkataa.

 

Amesema Harmorapa alikuwa ni mtu wa kumkimbiakimbia mpaka alipojaribu ku-force na kumhangaikia hadi imewezekana wao kuoana.

 

“Harmorapa alikuwa mtu wa kunikimbiakimbia siku zote mpaka nilipojaribu ku-force na kumhangaikia hatimaye imekuwa hivyo, alikuwa ananikataa kwa muda mrefu halafu haeleweki  ila nimetumia nguvu nyingi sana na kupambana ili kumpata ikiwemo pesa,” amesema.

 

Kwa upande wa Harmorapa amesema sababu ya kumkataa mwanzoni mwanamke huyo ni kutokana na uzuri wa rangi yake na alikuwa haamini.

 

Wanandoa hao wapya mjini wamesema wamemaliza fungate yao  na wapo tayari kujibu maswali ya watu ambao wanawauliza ikiwemo kufunga ndoa ya siri.

Leave A Reply