The House of Favourite Newspapers

Dai Risiti Popote Utakapotoa Fedha Kupata Huduma

0

DAI RISTI (2)
TUPO hapa kwa ajili ya kuiendeleza nchi yetu, kama tusipoiendeleza Tanzania, basi jua hakuna mtu atakayeweza kufanya hivyo, kama leo hautolia kwa ajili ya Tanzania, usifikiri kuna mtu atakuja kulia kutoka nchi nyingine.

DAI RISTI (1)Tunahitaji Tanzania ibadilike, hakuna atakayeweza kuibadilisha Tanzania isipokuwa Mtanzania mwenyewe. TRA ikishirikiana na Tanzania Youth Patriot (TYP) inakusisitiza ndugu Mtanzania kwamba popote utakaponunua kitu au kupata huduma fulani kwa gharama yoyote ile dai risiti.

DAI RISTI (3)Hii itaiwezeshesha serikali kupata kodi ambayo moja kwa moja itakwenda kufanya kazi katika jamii yetu. Kupitia hela hiyo, hospitali zitajengwa, watoto wataendelea kupata elimu bure, dawa zitaongezwa hospitalini na vitu vingine vyote kwa manufaa ya Watanzania wote.

Ndugu zangu, kumbuka kwamba mtu pekee anayeweza kuibadilisha Tanzania ni Mtanzania pekee na si mtu mwingine.

Bado tunahitaji vijana wengi wa kuibadilisha Tanzania yetu! Je upo tayari kuungana nasi?

Leave A Reply