Daimond Amshikia Panga Manaiki

Daimond Platnumz.

 

Na WAANDISHI WETU| RISASI JUMAMOSI| HABARI

DAR ES SALAAM: Ilitokea lakini haikuandikwa! Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ aliwahi kumshikia panga msanii wa filamu za Kibongo, Manaiki Sanga ikiwa ni baada ya kuombwa kufanya naye kolabo na kuchikichia fedha zake, Risasi Jumamosi lina habari kamili.

MANAIKI AVUJISHA MCHAPO Akizungumza na Risasi Jumamosi, Manaiki alisema uasama huo mpaka ukafikia kukimbizwa na panga na Diamond ilikuwa ni baada ya staa huyo kupokea fedha zake kwa ajili ya kushiriki kwenye wimbo wake wa Nafanya Mambo lakini akaingia mitini.

…AENDELEA KUTIRIRIKA Aliendelea kusema Diamond alikubali kwamba atashiriki kwenye wimbo

Manaiki Sanga.

huo na kuchukua fedha ya awali shilingi laki tatu lakini baada ya hapo aliingia mitini.

“Diamond alichukua fedha akaingia mitini akijua mimi ni mkulima kutoka shamba kwani hata nilivyomfuata sikumuonesha kuwa mimi ni mtoto wa mjini nilieleza tu shida yangu, kila nilivyokuwa nikijaribu kumpigia simu na kumueleza kuwa nimeshaandaa kila kitu sasa tuingie studio alisikiliza na kunipiga kalenda mwisho akawa hapokei simu kabisa.

“Nilipoona hapokei simu zangu nilifunga safari mpaka nyumbani kwao wakati huo alikuwa anaishi Sinza, nikamweleza mama yake akaniambia kuwa amesafiri amekwenda nje kwenye shoo lakini nisiwe na wasiwasi kazi itafanyika akirudi,” alisema Manaiki.

DIAMOND AMCHUNIA Diamond alirudi Bongo lakini hakumtafuta ili wafanye hiyo kazi ndipo Manaiki siku moja akasikia yupo kwenye kipindi cha redio Clouds FM, akaamua kumfuata na kumsubiri mpaka alipomaliza. “Alipotoka nilifuatana naye nyuma kwa nyuma kisha ‘nikablock’ huko barabarani alichofanya alijifanya anapotezea kisanii na kunichungulia kisha akaniambia usijali bwana tutaonana tutamaliza kazi yetu.

“Baada ya kusema vile akaondosha gari lake kwa kunidharau akidhani mimi nimemaliza kumbe nilikuwa na langu moyoni niliendelea kumfuatilia nikaenda ‘kumblock’ kwa mbele ili yeye anigonge lakini hakufanya hivyo.

DIAMOND AMTOLEA PANGA “Cha kushangaza Diamond badala ya kushuka tuzungumze ikibidi anilipe fedha zangu, alinitolea panga akiwa na washkaji zake kina Dimpoz kwa wakati huo ambao walikuja na kumsihi asinijeruhi.

Daimond Platnumz.

“Hata sikumuogopa tulipambana akatoa pesa akataka kunipa nikazikataa kwa sababu hayakuwa makubaliano yetu pale alinipa kwa kunidhalilisha, nikawaomba hata watu wangu wa karibu niliokuwa nao wasichukue kabisa nilitaka anirudishie kistaarabu kwani tulipeana kistaarabu, alisema Manaiki. MANAIKI APANGA MASHAMBULIZI Baada ya kuona amemdharau kisa anafedha alienda kupanga mashambulizi ambapo alitafuta vijana ambao yeye Diamond aliwahi kuwatumia kumteka Bob Juniour akawaeleza mchezo mzima wakampangia mkakati ambao aliingia moja kwa moja kwenye mtego.

Manaiki Sanga.

“Tuliamua kumtumia demu ambaye alitokea Mombasa akawa naye kimapenzi ndiyo hapohapo tukaenda kumbamba na kumshikisha adabu ambapo alitoa pesa zangu kistaarabu na faini juu tukamalizana, mpaka ninavyoongea na wewe hapa hata tukikutana hatusalimiani kabisa.”

DIAMOND ANASEMAJE? Mara baada ya kupata ubuyu huo ambao ulitokea lakini haukuandikwa, juzikati Risasi Jumamosi lilimsaka Diamond ili kumsikia anazungumziaje  tuhuma hizo ambapo alipopatikana, alikuwa na haya ya kusema: “Achana na huyo Manaiki kwa nini aibuke sasa hivi, hana ishu kabisa huyo.”

 

Save

Save


Loading...

Toa comment