The House of Favourite Newspapers

Daktari Aliyetoa Ushahidi Kilo Cha Naomi Alitishiwa Maisha

Familia ya Naomi Marijani, imeiomba serikali kuwaangalia kwa karibu mashahidi waliotoa ushahidi mahakamani kwenye kesi ya mauaji ya ndugu yao, wakieleza kuwa wengine walitishiwa maisha, akiwemo daktari aliyemfanyia vipimo mtuhumiwa ili kubaini kama wakati anatenda kosa hilo alikuwa na akili timamu.

Familia hiyo imeeleza kuwa taarifa zilizokuwa kwenye faili zilikuwa zimechakachuliwa ili kuonesha kama mtuhumiwa hakuwa na akili timamu lakini daktari akajitosa licha ya vitisho vyote na kufika mpaka jijini Dar es Salaam ambapo alienda kutoa ushahidi mahakamani uliowezesha haki ya ndugu yao kupatikana.