The House of Favourite Newspapers

Dakika 120 za Wanyarwanda Yanga zatikisa

WACHEZAJI wapya wa Yanga, Patrick Sibomana na Issa Bigirimana ambao wote ni raia wa Rwanda, wamekuwa kivutio katika kambi yao huko mkoani Morogoro.

 

Wachezaji hao ambao wamejiunga na Yanga msimu huu, wamekuwa kivutio kwa mashabiki wa timu hiyo waliojitokeza kushuhudia mazoezi yanayofanyika kwenye Uwanja wa Chuo cha Biblia, Bigwa
mkoani Morogoro.

 

Katika mazoezi hayo yanayofanyika asubuhi na jioni, yalianza juzi Jumatatu ikiwa ni maandalizi ya msimu ujao chini ya Kocha Msaidizi, Mzambia, Noel Mwandila.

 

Baada ya Yanga kwenda Morogoro, mazoezi ambayo yalikuwa gumzo ni ya juzi jioni ambayo walifanya kwa dakika 60 na jana asubuhi dakika 60 ambapo jumla walikuwa wamefanya kwa dakika 120.

 

Pamoja na wachezaji wengine waliopo kambini hapo, Wanyarwanda hao walikuwa kivutio kwenye mazoezi hayo ambapo walionekana kufanya mambo yao kwa ubora wa juu.

 

Bigirimana anatajwa kuwa mchezaji mahiri sana na alionekana kuelewa zaidi yale mazoezi ambayo yalikuwa yanatolewa na Kocha wa Yanga, Mwandila.

 

Mbali ya Bigirimana na Sibomana, wengine ni Mzambia, Maybin Kalengo na Mrundi, Mustapha Seleman, hawakuwa nyuma katika mazoezi hayo ambayo yamekuwa ni ya kujenga fi ziki za wachezaji kabla ya kuhamia kuchezea mpira.

 

“Hawa watakuwa bora sana kama muda mwingi wataanza kutumia mpira, nafi kiri tutaona ufundi wa juu,” alisema mmoja wa viongozi wa Yanga. Championi limewashuhudia wachezaji hao wakionyesha umahiri mkubwa katika mazoezi hayo huku wakionekana kuwa kivutio kikubwa kwa mashabiki.

 

“Haya ni mazoezi ya maandalizi ya msimu, mwalimu ndiyo ameanza na program ya kujenga timu ndiyo maana mazoezi yetu yamekuwa ya hivi kwa ajili ya kuweza kujenga fi ziki ya wachezaji.

 

“Hii imekuwa inafanyika asubuhi na jioni kutokana na maelekezo ya mwalimu, mwenyewe na ukiangalia wachezaji ambao wameanza unaona bado kuna kitu cha tofauti ambacho wanakifanya,” alisema mratibu wa timu hiyo, Hafi dh Saleh.

 

Wachezaji hao kwa sasa wanakula bata katika kambi hiyo kutokana na kulala kwenye hoteli ya kisasa iliyopo mkoani humo Morogoro.

Comments are closed.