The House of Favourite Newspapers

DAKTARI AANIKA MADHARA KUKATWA UTUMBO

KWA kipindi cha takribani wiki nzima sasa, gumzo kubwa katika ulimwengu wa mastaa ni kuhusu afya ya msanii maarufu Bongo, Wema Sepetu baada ya kusambaa video ikimuonesha akitoka kwenye hospitali moja jijini Dar ikidaiwa kuwa eti alikatwa utumbo ili kupunguza unene.

 

Video hiyo iliibua maswali mengi kuhusu kile kilichokuwa kikizungumzwa huku Wema akishindwa kujitokeza hadharani kueleza kilichompata na kama ni kweli alikatwa utumbo ili kupunguza unene ama ni maneno ya watu tu.

 

Aidha meneja wake, Neema Ndepanya alipoulizwa hivi karibuni kuhusu afya ya msanii wake huyo alipata kigugumizi licha ya siku chache nyuma kukiri staa huyo kusumbuliwa na tatizo la tumbo.

Hata hivyo, baada ya mengi kuzungumzwa, juzi Jumapili baada ya kupotea kwa muda mrefu, Wema aliposti picha ikimuonesha alivyo kwa sasa ambapo alionekana amepungua huku wengi wakimpongeza kwa muonekano wake.

Kufuatia upya huo wa Wema, baadhi ya wasichana waliomuona mtandaoni, walionesha kuvutiwanaye na wengine kudai kuwa, nao watafanya kila wawezavyo ikibidi kwenda kukatwa utumbo ili kupunguza unene.

 

“Jamani Wema kapendeza sana, licha ya kwamba kavaa dela (angalia picha ya mbele kushoto) lakini inaonesha kabisa amepungua tofauti na alivyokuwa huko nyuma. Sijui ndiyo huko kukatwa utumbo kama wanavyosema au kitu gani.

 

“Yaani ninavyotamani kupungua, na mimi nitafanya kila liwezekanalo ikibidi nitakwenda kukatwa utumbo maana naambiwa nayo ni njia mojawapo ya kupunguza unene,” alisema Sharika Sulle wa Sinza jijini Dar.

 

Baada ya kubainika kuwa baadhi ya wasichana walioona muonekano mpya wa Wema walishawishika kupunguza miili yao kwa kutumia njia zozote ikiwemo kukatwa utumbo, mwandishi wetu alimtafuta daktari maarufu jijini Dar, Godfrey Chale ambaye alifafanua kuhusu njia hiyo ya kupunguza unene.Kukatwa utumbo inakuwaje?

 

Kwa mujibu wa daktari huyo, njia hiyo ya kupunguza unene ambayo wengi huijua kama kukatwa utumbo kitaalum inaitwa Gastric Band ambapo sehemu ya tumbo la binadamu inabanwa ili kulipunguza ukubwa na kuruhusu kiasi kidogo cha chakula kuingia.

 

“Ni njia ya kitaalam ya kupunguza unene, kinachofanyika ni kupunguza ukubwa wa tumbo kwa kulibana katika sehemu ya juu ili mtu anapokula chakula kidogo tu ajisikie ameshiba. Hali hiyo humfanya kadiri siku zinavyokwenda kupungua unene,” alisema daktari huyo na kuongeza:

Image result for wema sepetu

“Ni njia inayoshauriwa kidaktari ya kupunguza unene lakini mbali na faida hiyo, kuna madhara yanayoweza kuwapata wanaofanya uamuzi huu.

“Kwa mfano, lengo lako linaweza kuwa ni kupungua lakini sasa ukakonda kupitiliza, hali ambayo pia kiafya siyo sawa. Lakini pia, tiba hii ya kupunguza unene inafanyika kwa kufanyiwa upasuaji ambapo damu nyingi inaweza kupotea na kusababisha madhara makubwa.

 

Madhara mengine yanayosababishwa na upasuaji huu, ni mwili kushindwa kuzikubali dawa za usingizi (Anasthetics) ambazo kwa kawaida mgonjwa yeyote anayefanyiwa upasuaji huchomwa kabla ya upasuaji. Hali hii ikitokea, maana yake ni kwamba mgonjwa anaweza kuzinduka wakati upasuaji ukiendelea na kusababisha kifo.

 

Matatizo mengine yanayoweza kusababishwa na upasuaji huu, ni mwili kupata mzio (allergy), kupata matatizo ya kupumua, damu kuganda kwenye miguu na kwenye mapafu, kuishiwa damu, kupata maambukizi kwenye damu na kupatwa na shambulio la moyo au kiharusi wakati wa upasuaji au baada ya kumalizika kwa upasuaji.

 

Pia kifaa maalum kinachowekwa tumboni baada ya upasuaji, kinaweza kuhama sehemu kilipowekwa au kikayeyuka na kusababisha madhara kwa mhusika, ambapo atalazimika kufanyiwa tena upasuaji. Utafiti unaonesha kwamba, kati ya asilimia 15- 60 ya watu waliofanyiwa upasuaji huu, hulazimika kufanyiwa upasuaji mwingine ili kurekebisha dosari zilizotokea awali.

 

Baada ya upasuaji, mhusika anatakiwa kufuata masharti ya vyakula, vinginevyo atatapika sana na kupatwa na tatizo la kutanuka kwa koo. Pia kifaa kinachoachwa tumboni, kinaweza kusababisha majeraha ya tumbo na viungo vingine vya ndani, husababisha kiungulia kikali, vidonda vya tumbo na maumivu makali ya tumbo.

 

Kutokana na madhara ya njia hiyo ya kupunguza unene, mastaa na watu wengine wanaotamani kupungua wameonywa kutoitumia ikiwa wana uwezo wa kutumia njia nyingine kama kufanya mazoezi, kufanya diet na nying

STORI: Mwandishi Wetu, Risasi Mchanganyiko

Comments are closed.