The House of Favourite Newspapers

Daktari Kizimbani kwa Kumbaka Mjamzito

0

Daktari wa Zahanati ya Lugunga Mkoani Geita Emmanuel Mpanduhi amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Bukombe kwa tuhuma za kumchoma sindano nne mjamzito mwenye umri wa miaka 20 na kisha kumbaka.

Daktari huyo anadaiwa kumbaka mjamzito January 15, 2020 saa saba mchana, baada ya mjamzito huyo kumueleza kuwa mimba yake ina miezi minne na ipo hatarini kutoka hivyo anaomba tiba ya kuzuia isitoke, akamchoma sindano na kumuingilia.

“Alimchoma sindano mbili mjamzito huyo, akamwambia aliyemsindikiza asubiri nje, akabaki na mjamzito chumbani akamchoma mbili nyingine kisha kumbaka,alipozinduka akajikuta amechafuka sehemu za siri na nguo ya ndani iko pembeni”-Orginess Digina, Mwendesha Mashtaka wa Polisi

Leave A Reply