The House of Favourite Newspapers

Daktari: Mama Mondi Ana Gonjwa Baya

0

PICHA ya chumbani aliyoiposti mitandaoni mama mzazi wa msanii, Nasibu Abdul ‘Diamond’ Sanura Kassim ‘Mama D’ ikionesha akiwa kitandani na mumewe aliyeonekana akiwa amelala kifua wazi ni kama imemponza mama huyo. 

 

Unajua kwa nini? Mara baada ya Mama D kuposti picha hiyo kwenye Instagram yake siku ya wapendanao ‘Valentine’ Februari 14, mwaka huu, watu walimjia juu wakimuona kama mtu fulani aliyepwaya kimaadili na kumkosoa vikali juu ya tabia yake ya kujifanya mtoto wakati yeye ni mtu mzima mwenye wajukuu.

 

Kufuatia michambo hiyo ya mitandaoni kuelekezwa kwa mama D, mwandishi wetu alimuuliza daktari maarufu jijini Dar es Salaam, Godfrey Chale kama mama huyo anaweza kuwa na shida katika tabia ambapo alisema:“Ana ugonjwa mbaya.”

 

“Kama jamii inamlalamikia kuwa matendo yake yamezidi kuwa ya ujana kuliko umri wake bila shaka kuna shida mahali fulanifulani katika tabia yake.

 

“Na unapozungumzia tabia ni vigumu kutofautisha na ugonjwa au tatizo jingine la kiafya, mtu anaweza kuugua tabia mbaya na akawa hawezi kujiponya.

 

“Chunguza walevi wa madawa ya kulevya, pombe, wavuta sigara na makundi mengine mabaya utagundua kabisa ni watu wanaohitaji tiba kama walivyo wagonjwa wengine wa malaria na kifua kikuu.”

ACHAMBUA UGONJWA WA TABIA

Sifahamu historia ya maisha ya mama Diamond kwa maana hiyo sitaki nimuongelee yeye badala yake nitaongelea zaidi tabia zilivyo na jinsi mtu anavyoweza kujisaidia.

 

“Umeniambia kuwa tabia za mama huyo zimekuwa zikiwashangaza wengi kutokana na jinsi anavyojiweka kama binti wa miaka 25, sitaki nimzungumzie yeye tu bali wote ambao tabia zao zinalaumiwa na jamii.

 

“Ukiona mtu mzima anafanya mambo ya ujanaujana kuna mambo mengi anaweza kuwa nayo likiwepo la kuruka hatua za ujana wake katika makuzi yake.

 

“Mara nyingi watu walioruka hatua (Stage) kwenye maisha yao tabia zao za ujanani au za utotoni ambazo hawakuzifanya huwa zinajirudia, jambo hili halina utafiti wa kitaalam lakini uchuguzi umeonesha hivyo,” alisema Daktari Chale.

 

Aliongeza kuwa, mabadiliko yasiyo ya kawaida ya tabia kwa binadamu.

(personality changes) hutokea kutokana na hali usiyoizoea katika maisha, ugonjwa au maumivu ya muda mrefu, mabadiliko haya pia huweza kusababishwa na magonjwa ya akili.

 

Alisema, ulevi au alcoholic addiction ni hali ya ugonjwa ambayo hubadilisha utendaji kazi wa ubongo na kuharibu uwezo wa ubongo “Neurochemistry.”

 

“Mabadiliko haya hubadilisha tabia ya mtu, mlevi hupatwa na sonona au Depression na mwili kuwa dhaifu, hukosa maamuzi na fikra na hujikuta anasemasema hovyo, kutumia maneno yasiyofaa na kudhalilisha mwili wake.

 

Dokta Chale alisema, kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na James Prochaska kwa kushirikiana na Carlo Diclemente wa Rhodes Island, katika miaka ya 1970, wakielezea mabadiliko ya kawaida ya mwanadamu yapo katika maeneo sita; ambayo huanza na kuendelea taratibu.

 

Hatua hizi kitaalamu tukianzia ya kwanza hadi ya sita ni: Precontemplation, Contemplation, Preparation, Action, Maintenance na mwisho Relapse.

PRECONTEMPLATION

Akifafanua zaidi daktari huyo alisema mara nyingi mtu aliyeko kwenye kundi hili huwa hakubali kama analo tatizo hata kama jamii ikimlaumu.

“Kwani kuna shida gani?”

 

“Kila anachofanya huona ni sahihi huenda hafahamu kama ni tatizo au siyo sahihi kutokana na wakati uliopo au mahali alipo au kwa umri alionao.

“Anakuwa hajajitambua kiasi kwamba wengine wakimtambua huweza kumuita mshamba au limbukeni.”

 

JINSI YA KUJIOKOA

Dokta Chale alisema inaweza kukosekana tiba ya moja kwa moja lakini mtu anaweza kulikabili tatizo hili kwa kujichunguza mwenendo wake.

 

“Unaweza kuangalia watu wa rika lako wanafanya kama wewe, ukiona hawafanyi na jamii inakushangaa, angalia madhara yake kwa jamii inayokuzunguka na kizazi chako, uwe mtu wa kukubali kukosolewa na kusemwa.

 

“Bahati mbaya watu wa kundi hili huwa na historia ya kutokuwa na mambo kwa msingi huo ukiona umeanza tabia ambayo hukuwa nayo lazima uwe makini.”

 

CONTEMPLATION

Aliongeza kuwa, hatua ya pili ya makundi ya watu ni wale ambao wako kwenye hatua hii kuanza kujitambua kutokana na wao wenyewe kujishtukia kutokana na kusemwa au kuelimishwa kuhusu mienendo yao.

 

“Wakianza kujitambua mgongano ambao hubaki nao ni wa fikra ‘conflicted emotions’ hivyo anashindwa kutoa maamuzi sahihi aache au aendelee anatakiwa asaidiwe kuacha vinginevyo atashindwa na kuendelea kuharibika.

 

CHA KUFANYA

Mtu aliyeko kwenye hatua hii anatakiwa aendelee kupima faida na madhara ya tabia hiyo kwa kizazi chake na jamii yake, ajihakikishie mwenyewe kuachana na tabia hizo na kuweka juhudi, achunguze vikwazo vinavyomkwamisha na aombe ushauri.

 

PREPARATION STAGE

Kuhusu hatua hii Dokta Chale alichambua kuwa ni ile hali ya mtu kujua tabia yake kuwa ni tatizo na anajaribu kuacha na kuanza kuona mabadiliko kidogo.

“Ukiona tayari unajiona kuwa una shida katika tabia zako na umeanza kuziacha kidogokidogo usikate tamaa.

 

“Ukianza kuona heshima yako kwenye jamii inarudi basi weka malengo yako mazuri kwa kuandika, andaa mpango mkakati wa kudumu hivyo na tumia njia mbalimbali za kupunguza mambo yanayokuletea changamoto hizo na uyaondoe.

 

“Hatua hii ni kwa tabia yoyote iwe uvutaji sigara,ulevi au tabia yoyote mbaya inayokufanya uonekane kituko kwenye jamii.”

 

ACTION (MATENDO)

Hatua ya nne ambayo mtu anaweza kuifikia katika kujitoa kwenye gonjwa la tabia mbaya ni kukaza katika matendo mazuri uliyopanga kuyaishi.

 

“Ukiona malengo ya kuachana na tabia zinazoshangaza jamii yako na kukuvunjia heshima bado yana vikwazo omba ushauri na msaada kwa watu wanaokuzunguka wenye mapenzi mema na wewe.

 

Hii ni hatua ya kudumu katika tabia mpya njema, hapa ni kuhakikisha unaachana kabisa na yaliyopita “the past is over” usipende kuyakumbuka katika kipindi kifupi ulichotoka kwani unaweza kukumbushia enzi.

EPUKA VISHAWISHI vitakavyokurudisha ulipotoka. Daima jenga tabia ya kujisifu na kujionyesha mfano bora wa mabadiliko kwa wenye tabia kama ulizokuwa nazo.

 

RELAPSE

Ni mlipuko wa tabia ileile, baada ya kuacha kwa muda halafu unarudi tena kulekule tena kwa nguvu zaidi au kwa kujifichaficha.

 

Hii ni kutokana na kukatishwa tamaa na kukosa ushirikiano na jamii au ndugu au ‘disappointment’, kuvurugikiwa ’frustation’ kwa kuona unapobadilisha tabia mambo yako hayaendi, unapoteza marafiki uliokuwa nao zamani.

 

“Wakati mwingine kubaliana na hasara za kuachana na tabia mbaya kwani unaweza kujikuta ukianza safari ya kutafuta marafiki wapya kutokana na wale wa zamani kukuona kama umekuwa mshamba,” alisema Dokta Chale.

Stori: Mwandishi wetu, Amani

Leave A Reply