The House of Favourite Newspapers

Daktari wa Liverpool kumtibu beki wa Simba

0

KOCHA wa Simba, Dylan Kerr hajaridhishwa na kitendo cha beki wake Emily Nimubona kuvishwa plasta ngumu (POP) kiganjani badala yake anataka utumike utaalam kutoka Liverpool kumtibu.

Nimubona ambaye ni beki wa kulia raia wa Burundi, juzi alivunjika mfupa wa kidole cha mwisho mkono wa kulia na amevishwa POP katika kiganja chote.

“Haiwezekani wamvishe POP katika kiganja chote, huyu atachelewa kupona hivyo inatakiwa ipatikane njia nyingine ambayo si lazima itumike hii,” Kerr raia wa Uingereza aliliambia Championi Jumamosi na kuongeza:

“Kwetu Uingereza kuna utaalam unatumika katika kutibu jeraha kama hili, nitawasiliana na daktari wa kule ili amuelekeze daktari wetu.”

Kerr anafahamika kuwa na ukaribu na aliyekuwa kocha wa Liverpool, Brendan Rodgers pia ana marafiki kadhaa katika Jiji la Liverpool, amethibitisha msaada huo ataupata kutoka jijini humo.

Daktari wa Simba, Yassin Gembe alipotakiwa kutoa ufafanuzi alisema: “Kilichofanyika ndicho kilichopaswa, nimemsikia kocha  na nitafanya kama anavyotaka haina shida nitafuata maelekezo.”

Emily atakuwa nje ya uwanja kwa wiki nne. Majeruhi wengine  wa Simba ni Hamis Kiiza anayeuguza nyama za paja pamoja na Mohamed Fakhi aliyeumia goti.

Leave A Reply