The House of Favourite Newspapers

DAKTARI WA NAMIBIA ALIYEMTUNUKU MBOSSO

Coleen Tjikune maarufu kwa jina la Chikune.

UNAWEZA ukawa hujawahi kumsikia kwa kuwa siyo maarufu sana hapa nchini Tanzania kama walivyo wasanii wengine wa nje ya nchi, lakini nikujuze tu kuwa, mwaka 2016 alich-ukua Tuzo ya Msanii Bora wa Kike wa Namibia.

 

Huyo ni Coleen Tjikune maarufu kwa jina la Chikune, mwa-na-mama huyu anafa-nya Muziki wa Afro Pop akitokea nchini Namibia na hivi karibuni ameba-hatika kufa-nya kolabo na msanii wa Bongo Fleva kutoka Lebo ya WCB, Mbwana Yusufu Kilungi ‘Mbosso’, wimbo wao ukitambuilika kwa jina la Pieces.

 

Championi Ijumaa lilimtafuta mrembo huyo na kufanya naye mahojiano maalum (exclusive interview) ili kufahamu vitu vingi kutoka kwake kuhusu muziki na maisha yake kiujumla.

Chikune akiwa na Mboso

Mrembo huyo mwenye umri wa miaka 26, amefanya mahojiano haya kwa njia ya simu akiwa kwao Namibia, ikiwemo suala la kuamua kumtunuku heshima msanii wa Tanzania kufanya naye kazi kwenye wimbo wake, huyu hapa anafunguka:


CHAMPIONI: UNA MUDA GANI TANGU UMEANZA MUZIKI?

 

CHIKUNE: Nimeanza muziki tangu nikiwa mdogo, nilikuwa naimba lakini kujulikana kwenye ‘game’ siyo muda sana, ni kama miaka mitatu au minne iliyopita.

ULIFAHAMIANA VIPI NA MBOSSO MPAKA KUFIKIA KUFANYA KOLABO?

CHIKUNE: Nilimfahamu Mbosso kupitia Diamond, alipofika Namibia kutumbuiza ndiyo tukazungumza vitu vingi sana kuhusu soko la Tanzania lilivyo na Namibia. Nilipata nafasi ya kumsikilizisha wimbo wangu huu unaitwa Pieces, akashangaa sana nimeimba Kiswahili, ndiyo akanishauri nifanye Remix na Mbosso, nikamchunguza nikaona ni mtu ambaye anakuwa vizuri kwenye soko la muziki, tukafanya kazi.

 

KOLABO YAKO NA MBOSSO IMEKUSAIDIA CHOCHOTE?

CHIKUNE: Imenisaidia sana kufahamika nchini Tanzania ndani ya muda mfupi na hata mipaka ya Tanzania pia, naweza nikasema nimepiga hatua fulani, namshukuru sana kwa sababu amefa nya kama nilivyotaka.

 

NI MSANII GANI MWINGINE KUTOKA TANZANIA AMBAYE UNATAMANI KUFANYA NAYE KAZI?

CHIKUNE: Wapo wengi akiwepo Diamond mwenyewe, Vanessa Mdee, Rayvanny na kijana anaitwa Brian Simba ambaye ni mpya kwenye muziki lakini anafanya vizuri, ni hao ambao niliwafikiria kwa haraka kufanya nao kazi hivi karibuni.

 

NI VITU GANI ULIJIFUNZA KUTOKA KWA MBOSSO?

CHIKUNE: Nimefurahi sana kuniuliza hili swali kwa sababu nilitamani niseme vitu ambavyo nimejifunza kutoka kwake ambavyo ni vingi sana, kwanza ni mtu mwenye njaa ya mafanikio, ana bidii katika kazi yaani natamani siku moja nije kuwa kama Mbosso.

“Amenipa hamasa sana ukizingatia maisha aliyopitia lakini bado ameweza kupambana kufikia mafanikio aliyonayo.

MUZIKI UNALIPA NCHINI NAMIBIA?

CHIKUNE: Ndiyo unalipa kama unaufanya kwa bidii kubwa na kama ukiufanya kuwa biashara, tatizo huwa ni nchi yangu ni ndogo sana, tupo milioni tatu tu kwa hiyo soko ni dogo halafu changa, ndiyo maana nikaona nifanye kolabo za nje ili kuuvusha muziki wangu uweze kupenya kwenye boda ya nchi mbalimbali. Ila kwa ufupi muziki unalipa kiukweli.

 

NI CHANGAMOTO GANI UMEIPATA KUFANYA KAZI NA MBOSSO?

CHIKUNE: Hakuna changamoto niliyoipata kwa sababu ni mstaarabu sana, mnyenyekevu na nilipenda jinsi alivyo.

Labda changamoto ambayo niliiona ni kutoka Namibia kuja Tanzania kushuti video ya wimbo wetu (Pieces Remix) ilitakiwa nipange muda ambao haitaingiliana na ratiba za Mbosso kwa hiyo ikabidi nivunje baadhi ya ratiba zangu ili nije kushuti.

 

UMEOLEWA NA UNA WATOTO WANGAPI?

CHIKUNE: Maisha yangu binafsi yanamkanganyiko sana na ndiyo maana nimeamua kutozungumzia chochote ili kulinda mambo yangu ya faragha.

ULIPATA CHANGAMOTO YOYOTE WAKATI UNAJIFUNZA KUZUNGUMZA MANENO YA KISWAHILI ULIYOYATUMIA KWENYE WIMBO WAKO?

 

CHIKUNE: Sikupata changamoto kujifunza lakini changamoto ilikuwepo pale ambapo ilitakiwa niyatamke yale maneno kwa ujasiri na usawa huku yakiendana na hisia zangu, jambo ambalo lilinifanya nirekodi mara mbili mpaka nikapatia.

 

NJE YA MUZIKI UNAFANYA SHUGHULI GANI?

CHIKUNE: Mimi ni mwanafunzi wa udaktari na ndiyo maana kuna muda nakuwa bize nashindwa kufanya kazi zangu za muziki

Makala na Shamuma Awadhi, Championi Ijumaa

Comments are closed.